Mwandishi wetu
TIMU ya Tanzania ya soka ya wanawake umri chini ya miaka 20 leo itashuka uwanjani katika mji wa Benin City kupambana na wenzao wa Nigeria, Falconets katika mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Ufaransa.
Msafara wa timu ya tanzania wenye wachezaji 20 uliondoka Alhamisi usiku kuelekea Abuja on Thursday kabla ya kuunganisha safari kwenda Benin City kwa mchezo wa leo.
Waamuzi waliochaguliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) kuchezesha pambano hilo ni Vincentia Enyonam Amedome wa Togo atakayekuwa katikati, akisaidiwa na
Kossiwa Kpadenou na Abra Sitsope Agbedanou huku Aissata Ameyo Amegee akiwa mwamuziki wa nne.
Kamishina na mechi ni Rochell Woodson kutoka Liberia.
Kabla ya kuondoka nchini kocha wa timu hiyo Sebastian Nkoma alisema wana matumaini ya kufanya vema kwenye mchezo wa leo huku nahodha wa timu hiyo, Wema Richard akisema wanatumiani kushinda na kurudi na ushindi , kauli mbiu yao ni “Hapa ni kazi kazi.”
Kikosi cha wachezaji 20 wa Tanzanite kilichoko Nigeria ambacho kutoka humo kocha Nkoma atachagua timu yake ya wachezaji 11 na wa akiba ni makipa watatuAgatha Joel, Zainab Abdallah na Gelwa Mgomba, walinzi; Eva Jackson, Aquila Gasper, Asphat Kasindo, Ester Mayala, Silivia Mwacha, Stella Wilbert, Wema Richard, Hadija Ali, Rukia Anafi na Christine Daudi.
Viungo ni Herieth Shija, Julieth Singano na Shamimu Hamis na Washambuliaji ni Veronica Mapunda, Opa Clement, Zainabu Mohamed na Philomena Daniel.
Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika Oktoba Mos kwenye uwanja wa Chamazi.
Mshindi katika mechi mbili za timu hizo atapambana na
mshindi kati ya Morocco na Senegal katika mzunguko unaofuata Novemba mwakani.

Comments
Post a Comment