Skip to main content

Tamasha la Tigo Fiesta laacha gumzo Mara

Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa(aliyevaa koti la suti) akicheza mziki wakati wa uzinduzi wa tamasha la Tigo Fiesta, kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani humo usiku wa kuamkia jana .

Mwandishi Wetu, Mara

WAKAZI wa mji wa Musoma wamelipokea tamasha la Tigo Fiesta 2017 kwa furaha kubwa baada ya kulikosa mwaka jana.
Akifungua tamasha hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk. Charles Mlingwa alisema hiyo ni fursa ya pekee kwa tamasha hilo kufanyika mkoani mwao tena kwa upendeleo wa kuwa mkoa wa pili baada ya Arusha.

Msanii wa nyimbo za kitamaduni Saida Karoli, akitumbuiza kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma Mkoa wa Mara,kwenye tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana .

 ''Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru Tigo na Clouds Media kwa kutuletea fursa mkoani kwetu, najua wakazi wa Musoma mmefaidika sana kwenye biashara mbalimbali, naomba niwahakikishie leo mtaburudika na mtaondoka salama kwa ulinzi tuliweka, alisema Mlingwa.

Msanii Coyo aliamsha mashabiki waliofurika uwanja wa Karume mjini hapa kwa kupanda jukwaani na kuwafanya wapagawe na nyimbo zake akifuatiwa na Nandy.
Wasanii wa muziki wa rap Roma Mkatoliki na Stamina (Rostam) ndio waliibeba Tigo Fiesta vilivyo walipoimba pamoja ikiwemo wimbo wao mpya 'Huku au Kule' na kushangiliwa kwa nguvu na mashabiki.
Roma Mkatoliki na Stamina wakifanya yao.
Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Edgar Mapande alisema Tigo imedhamini tamashahilo mwaka huu ili kuendeleza na kukuza vipaji vya wasanii na kuwaletea wateja  burudani,  ikiwa ni  kurudisha kwa jamii inachopata.
Alisema Tigo imepeleka huduma za intaneti kwenye shule kadhaa ili kuwasaidia  wanafunzi  wa  shule  za  sekondari  kusoma  kwa  njia  ya  mtandao,   ambayo  imeanza  kunufaisha  shule  mbalimbali 
Kwa upande wa mashabiki Michael Joseph mkazi wa Tarime alisema aliamua kukusanya fedha kidogo kidogo ili aje aone tamasha hilo, amefurahi kutimiza dhamira yake kwa kuona wasanii mbalimbali wakitumbuiza.
Jumla ya wasanii 17 walipanda jukwaani wakiwemo 
Nandy, Ditto, Benpol'Jux, Saida, Joh, Darassa, Roma, Blue, Fid Q, Stamina, Chege, Shilole, Dulla Makabila Adam Mchomvu, Coyo na Future. 

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...