Skip to main content

Taifa Stars, Botswana ngoma uwanjani


Kocha Salum Mayanga (kushoto) akiwa Msemaji wa TFF, Alfred Lucas

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesema maandalizi ya mchezo kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Botswana utakaofanyika kesho kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam yamekamilika ikiwa ni pamoja na kwa timu pinzani.

Akizungumza Dar es Salaam, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema maandalizi kwa kiasi kikubwa yamekamilika  ikiwa ni pamoja an wachezaji wanaocheza nje wa Taifa Stars kuwasili pamoja na  timu ya Botswana kwa Shirika la Ndege la Kenya (KQ) usiku wa jana na kufikia Hoteli ya Urban Rose iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Wachezaji wa Stars wanaocheza soka ya kulipwa nje waliowasili ni  Simon Msuva kutoka Klabu ya Difaa El Jadidah ya Morocco,  Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk ya Ubelgiji), Elias Maguli (Dhofar FC ya Oman), Abdi Banda (Baroka FC ya Afrika Kusini), Hamis Abdallah (Sony Sugar ya Kenya)  na Farid Mussa wa CD Tenerif ya Hispania.
Alisema Orgenes Mollel wa FC Famalicao ya Ureno ameshindwa kuwasili kutokana kushindwa kukamilisha mchakato wa kupata vibali vya kumwezesha kusafiri kutoka Ureno na kurejea bila ya matatizo.
Wachezaji wa Stars wengine walioko kambini ni  Dar es Salaam ni walinda mlango; Aishi Manula (Simba), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Yanga).
 Walinzi ni Gadiel Michael (Yanga), Boniface Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Yanga), Salim Mbonde (Simba) na Erasto Nyoni (Simba).
Viungo ni Himid Mao – Nahodha Msaidizi (Azam FC), Mzamiru Yassin (Simba), Said Ndemla (Simba), Shiza Kichuya (Simba), wakati Washambuliaji ni Raphael Daud (Yanga), Kelvin Sabato (Azam FC) na Emmanuel Martin (Yanga).
Viingilio  vya mchezo huo vitakuwa ni  sh. 10,000 kwa Jukwaa Kuu na Sh 5,000 kwa mzunguko.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...