![]() |
| Mwenyekiti wa Klabu ya Majimaji, Steven Ngonyani (kulia) na Mratibu wa Sokabet, Franco Ruhinda wakisaini mkataba wa kuidhamini Majimaji Dar es Salaam leo |
KAMPUNI ya Sokabet imejitosa katika udhamini kwa timu ya Majimaji ya Songea (Wanalizombe) ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania.
Udhamini huo una thamani ya sh. milioni 150 utakaodumu kwa mwaka mmoja.
Akizungumza wakati wa kutiliana saini makubaliano hayo jana jijini Dar es Salaam, mwakilishi wa Sokabet nchini, Franco Ruhind alisema lengo la kampuni hiyo ni kuleta mapinduzi makubwa katika soka nchini.
"Tanzania ni nchi inayopenda soka, hivyo kwa kulitambua hilo tumeona kama Sokabet kuanza kuleta mapinduzi katika michezo kupitia udhamini huu kwa klabu ya Majimaji wa sh. milioni 150 kwa mwaka mmoja," alisema Ruhinda.
Aidha alisema ufadhili huo ni sehemu ya kurudisha sehemu ya faida wanayopata kwa jamii inayowazunguka ili kuwanufaisha kupitia soka, imekuwa ikitoka ajira kwa vijana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sokabet, Shane Leahy alisema ufadhili huo ni mwanzo tu katika kuleta maendeleo ya soka kupitia klabu hiyo na kubainisha kuwa watafanya mambo mengine makubwa zaidi.
Mwenyekiti wa Majimaji Steven Ngonyani alishukuru kwa udhamini huo wa Sokabet na kuahidi klabu hiyo kufanya vizuri katika msimu huu na kuhakikisha wanachukua ubingwa.
Naye, Dani Mrwanda akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake alisema wamefurahishwa kwa ufadhili huo na kusema wanadeni kubwa kwa viongozi na wanasongea na kuahidi kupambana na kufanya vizuri ili kuwafurahisha mashabiki na wapenzi wa Majimaji.

Comments
Post a Comment