Skip to main content

Sloane Stephens awa bingwa Tenisi wanawake Marekani, atwaa bilioni 8.4/-

Sloane Stephens akifuarahi baada ya kukabidhiwa Kombe la Ubingwa wa tenisi kwa wanawake katika mashindano ya Marekani baada ya kumfunga kwa seti 2-0 Madison Keys kwenye uwanja wa Flushing Meadows.


NEW YORK, Marekani
SLOANE Stephens amekuwa bingwa mashindano ya Tenisi ya Marekani 2017  kwa upande wa wanawake baada ya kumshinda kwa seti 2-0 mmarekani mwenzie, Madison Keys katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Flushing Meadows.


Sloane Stephens akionekana kwua na hisia baada ya kupwa hundi inayoonesha amepata zawadi  ya pauni pauni milioni 2.84 ambazo ni sawa na zaidi ya sh. bilioni 8.4 kwa kutwaa ubingwa wa Tenisi Marekani kwa wanawake.

Stephens ambaye  katika viwango vya ubora wa tenisi vya dunia anashikilia namba 83 alimzidi mpinzani wake wakati wote wa mchezo  na kupata alama 6-3, 6-0 .
Kwa kutwaa ubingwa huo, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza ambaye yuko chini kwenye viwango vya ubora kufika fainali na kutwaa ubingwa wa mashindano hayo. Kwa mara ya mwisho aliyefanya hivyo alikuwa ni Clijsters  2009 alitwaa ubingwa baada ya kujifungua  na kuwa na mtoto.



Sloane Stephens (kushoto)  akipongezana na Madison Keys baada ya mchezo kuisha.


Stephens pamoja na kupata kombe 'ametajirika' kwa kupata zawadi ya pauni milioni 2.84 ambazo ni sawa na zaidi ya sh. bilioni 8.4.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 alianza kucheza katika mashindano ya tenisi ya Wimbledon baada kutocheza msimu mzima uliopita kutokana na kupata ufa katika mguu wake.
Alitumia saa moja na dakika moja, kushinda mchezo wake wa fainali dhidi ya mpinzani wake Madison Keys  ambaye pia ni rafiki yake.
Stephens, ambaye kabla ya kuwa namba 83 kwa ubora alikuwa namba 934 wiki tano zilizopita,  alisema: Ni kitu cha kusisimua, nilifanyiwa upasuaji Januari 23 na kama kama angetokea mtu na kuniambia nitakuwa bingwa wa Tenisi Marekani ningesema haiwezekani. 
Keys alimpongeza  Sloane ambaye alimwelezea kwua ni rafiki yake wa karibu, kwa kutwaa ubingwa huo na kusema katika mchezo wa fainali hakucheza kwa kiwango chake kizuri, amefurahia ushindi wa mpinzani wake.
Hata hivyo kwa kuwa mshindi wa pili katika mashindano hayo hajaondoka mikono mitupu. Amepata kombe na fedha dola za Marekani, 1,825,000 ambazo wa fedha za Tanzania ni zaidi ya sh. bilioni 4.




Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...