Skip to main content

Simba yaipa kibajaji Mwadui, Bocco akifungua akaunti




SIMBA baada ya kutoka suluhu dhidi ya Azam FC katika mchezo wake wa mzunguko wa pili, imerudishaa dozi yake ya kufunga mabao kwa kuilaza mabao 3-0 (kibajaji) Mwadui FC kweney Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Kiganda,  Emmanuel Okwi alionesha umuhimu wake katika kikosi cha Simba kwa kufunga mabao mawili katika ushindi huo na kufanya afikishe mabao sita katika mechi mbili alizocheza.

Kwenye mchezo uliopita dhidi ya Azam, Okwi hakucheza kwa kutokuwa fiti baada ya kutoka kuitumikia timu yake ya taifa ya Uganda iliyokwenda kucheza dhidi ya Misri na kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia. 

Katika Mchezo wa kwanza dhidi ya Ruvu Shooting iliyoshinda mabao 7-0. Okwi alifunga manne.

Okwi jana alifunga mabao hayo dakika ya saba baada ya kupata pasi kutoka Shiza Kichuya na jingine  dakika 67 baada ya kuwatoka walinzi wa Mwadui.

Bocco ambaye amesajiliwa Simba msimu huu akitokea Azam FC, jana aliosha nyota yake kwa kufunga bao lake la kwanza zuri msimu huu kwenye timu hiyo, dakika ya 72, baada ya kumpiga chenga mlinzi wa Mwadui.

Kwa ushindi huo Simba imefikisha pointi saba na kuwa ya pili  sawa na Azam FC iliyopo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo nyuma ya Mtibwa yenye pointi tisa baada ya kushinda michezo yake yote mitatu iliyoanzia nyumbani. Mwadui ina pointi tatu.

Katika mchezo ujao Simba itacheza ugenini Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza dhidi ya Mbao FC, Sptemba 21, mwaka huu huku mwadui ikiikaribisha Tanzania Prisons siku hiyo Uwanja wa Mwadui Complex.

 Simba; Aishi Manula, Ally Shomari, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Salim Mbonde, James Kotei, Emmanuel Okwi, Muzamil Yassin/Jonas Mkude, John Bocco, Nicholas Gyan/Mwinyi Kazimotona Shiza Kichuya/Laudit Mavugo.

Mwadui FC; Arnold Massawe, Malika Ndeule, David Luhende, Revocatus Mgunga, Abdallah Mfuko, Razack Khalfan, Abdallah Seseme, Awadh Juma/Uwesu Ally, Evarist Mjwahuko, Gerald Mathias/Benedicto Mwampyate na Hassan Kabunda.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...