![]() |
| Ronney alipokuwa akiwasili mazoezini leo. |
LONDON, Uingereza
Wayne Rooney hatimaye amekutana uso kwa uso na kocha wa Everton, Ronald Koeman katika mazoezi leo kwa mara ya kwanza tangu akutwe na mkasa wa kukamatwa na polisi akiendesha gari huku akiwa amelewa pombe.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema klabu yake imemtoza faini ya mshahara wake wa wiki mbili kiasi cha pauni 230,000 ( zaidi ya sh. milioni 668) kutokana na kitendo hicho.
![]() |
| Rooney na mkewe Colleen enzi mambo yao yalipokuwa safi. |
Rooney alikamatwa na polisi akiwa anaendesha gari la mwanamke aina ya VW Beetle karibu na eneo analoishi la Cheshire baada ya kunywa pombe nyingi kwenye klabu ya usiku.
![]() |
| Rooney akishan akilishia moja ya mabao aliyofunga baada ya kurejea Everton akitokea Manchester United aliyoichezea kwa miaka 13. |
Kutokana tukio hilo mkewe, Colleen ambaye ni mama wa watoto wake watatu ameondoka nyumbani kwake na kwenda kwa wazazi wake akiwa na watoto.
Kutokana na kukamatwa kwa kesi yake imepangwa kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Hakimu mkazi ya Stockport Septemba 18, mwaka huu.
Rooney anatarajiwa kurejea Old Trafford kucheza na timu yake ya zamani ya Manchester United siku moja kabla ya kusikilizwa kesi yake .



Comments
Post a Comment