Skip to main content

Ronaldo, Casilas wavunja rekodi Ligi ya Mabingwa

Cristiano Ronaldo  akishangilia moja ya mabao yake aliyofunga usiku wa kuamkia leo.

MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo amerejea kwa kishindo katika timu ya Real Madrid baada ya kutoichezea katika Ligi Kuu Hispania akitumikia adhabu ya kukosa mechi tano kutokana na hatia ya kumsukuma refa katika mchezo dhidi ya Barcelona kwa kuifungia mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Apoel Nicosia katika mchezo wa  Ligi ya Mabingwa, huku akiendelea kuvunja rekodi katika mashindano hayo .
Ronaldo aliifungia Real ambao ni mabingwa watetezi mabao hayo dakika ya 12 na 51, la kwanza akifunga kwa shuti la karibu na la pili kwa penalti.
Mlinzi Sergio Ramos alifunga bao la tatu kwa tiktak.

Iker Casillas

Real Madrid imeshinda mchezo wake wa kwanza katika mashindano hayo ikicheza uwanja wa nyumbani kati ya mara 11 ilizocheza.
Cristiano Ronaldo ameweka rekodi ya kufunga mabao 55 nyumbani ambayo ni mengi kuliko mchezaji yeyote  katika Ligi ya Mabingwa huku Lionel Messi akimfuatia kwa kufunga mabao 54.
Ronaldo pia amefunga penalti nyingi zaidi 12 katika mashindano huku Messi akifunga 11.
Kwa matokeo hayo timu ya Real inayonolewa na Zinedine Zidane imekuwa kinara katika Kundi H kwa tofauti ya mabao na  Tottenham, ambayo iliifunga Borussia Dortmund mabao 3-1.
Timu ya Besiktas ya Uturuki imekuwa kinara katika Kundi G baada ya kushinda mabao 3-1 ugenini dhidi ya Porto. 
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, timu iliyofika nusu fainali katika mashindano yaliopita Monaco ilitoka sare ya bao  1-1 dhidi ya timu ngeni kwen ye mashindano hayo RB Leipzig.
Mlinda mlango wa Porto, Iker Casillas ameifikia rekodi iliyowekwa na  mchezaji wa zamani wa Manchester United, Ryan Giggs kwa kucheza katika mashindano 19 na kucheza na timu nyingi 53, tofauti kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa.
Katika uwanja wa Anfield, Liverpool imejikuta ikishindwa kuibuka na ushindi baada Joaquin Correa kufunga bao la kusawazisha na kufanya Sevilla itoke sare ya mabao 2-2 dhidi ya wenyeji wao.
Pia katika mchezo huo, Liverpool ilipata penalti lakini lakini  Roberto Firmino alipiga nje.
Wageni walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Wissam Ben Yedder , kabla ya Firmino na Mohamed Salah kufunga kwa upande wa wenyeji.
Katika mchezo huo, kocha wa Sevilla, Eduardo Berizzo alitolewa uwanja kwenda kuka ana mashabiki kutokana na kunyanganya mlinzi wa Liverpool,  Joe Gomez mpira wakati wa kurusha.
Katika mchezo wa Kundi F, timu ya Manchester City ikiwa ugenini, ilipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi Feyenoord ya Uholanzi mjini Rotterdam.
Mabao ya City yalifungwa na  Stones (dk. 2, dk 63), Agüero (dk.10) na Jesus (dk.25)
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, Shakhtar Donetsk iliifunga Napoli mabao 2-1.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...