MADRID,Hispania
MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo amerejea katika timu ya Real Madrid akitokea kuitumikia timu yake ya Taifa ya Ureno na kuonesha gari lake jipya la kifahari aina ya Ferrari F12.
Nyota huyo ametumia mtandao wa kijamii kuweka picha inayomwonesha akiwa amesimama kando gari lake hilo jipya lenye thamani ya pauni 350,000 ambazo ni zaidi ya sh. trilioni moja huku mtoto wake wakiwa kwenye usukani.
Gari hilo linatajwa kuwa na kasi kubwa, linaweza kusafiri umbali km 211 kwa saa(ni zaidi ya umbali wa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ambao ni km 193.63 .
Ronaldo ana ulevi wa kupenda magari ya kifahari, miongoni mwa magari yake mengine anayoyamiliki ni Bugatti Veyron na Mercedes.
Amelionesha gari lake hilo jipya baada ya kuitumikia timu yake ya Ureno katika mashindano ya kimataifa .
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United aliifungia nchi yake mabao matatu
hat-trick wakati nchi yake ilipocheza na Faroe Islands na kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 na kutoa pasi ya bao kwa Andre Silva katika ushindi wa bao1-0 dhidi ya Hungary.
Pamoja na kupata ushindi katika mechi hiyo mbili, Ureno iko nafasi ya pili kwenye Kundi B Nyuma ya Uswisi katika mbio za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia, kama ikibakia katika nafasi hiyo hadi mwisho italazimika kucheza mechi ya mchujo.
Ronaldo anatarajiwa kurejea mazoezini katika timu ya Real Madrid wakati wowote , hatacheza mechi za ligi tatu baada ya kupewa adhabu ya kutocheza mechi tano kwa kosa la kumsukuma refa uwanjani wakati timu yake ikicheza na Barcelona.

Comments
Post a Comment