RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameunda Kamati ambayo itakuwa na jukumu la kuwachagua wachezaji watakaokuwa wakipata tuzo mbalimbali katika Ligi Kuu ya Vodacom (VPIL) Tanzania Bara msimu wa 2017/18.Kamati hiyo imejumuisha wadau mbaliambali wa michezo wakiwemo viongozi na waandishi wa habari za michezo.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho hilo,, Alfred Lucas, leo kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Ahmed Mgoyi wakati Makamu Mwenyekiti ni Almas Kasongo ilihali Amiri Mhando ameteuliwa kuwa Katibu wa kamati hiyo ya tuzo.Mhando ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na Mhariri wa Gazeti la Spotileo.Wajumbe wa kamati hiyot ni Ibrahim Kaude; Mkuu wa Kitengo cha Michezo katika Kampuni ya Azam Media, Patrick Kahemele na Kocha wa soka, Kenny ‘Mzazi’ Mwaisabula.Wengine ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Uchapishaji ya Global (Global Publisher inayochapisha magazeti kadhaa likiwamo Championi), Saleh AllyMta; ngazaji mahiri wa michezo kutoka Kituo cha Redio cha EFM, Ibrahim Masoud na Mtangazaji wa Vipindi katika Kituo cha Radio ya Watu, Fatma Likwata.Pia wamo Mwandishi Mwandamizi wa Michezo wa Gazeti la Mwanaspoti linalochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communication (MCL), Gift Macha; Katibu Mkuu wa Chama cha Wachezaji wa Mpira wa Miguu, Said George na Mhariri wa Michezo wa Gazeti la HabariLeo linalotolewa na TSN, Zena Chande.
WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Comments
Post a Comment