![]() |
| Kim Jong akiwa ametupia jezi ya Manchester United |
Pyongyang, Korea Kaskazini
RAIS wa Korea Kaskazini ambaye kwa siku za karibuni amekuwa akitumishiana kifua na Marekani akitamba nchi yake ina uwezo mkubwa wa kijeshi na kwamba iko tayari kupambana nayo, Kim Jong amebainika ni shabiki wa kutupwa wa timu ya Manchester United .
Rais huyo anasema bado siku kidogo tu wachezaji wa Korea Kaskazini wataanza kucheza sehemu mbalimbali duniani ikiwemo katika Ligi Kuu England.
Rafiki wa karibu wa rais huyo ambaye anatamba kuwa nchi yake ina silaha nyingi za nyuklia na iko tayari kuzitumia kama ikichokozwa ameiambia SunSport kuwa, mshikaji wake huyo anapenda soka nzuri na huwa hakosi kutazama mechi kubwa mashindano makubwa.
![]() |
| Kikosi cha Man United |
Seneta wa Italia, Antonio Razzi amethibitisha kuwa aliwahi kuambiwa na Kim katika mazungumza yao binafsi kwamba anaipenda timu ya Mashetani Wekundu.
Alipouuliza Kim anajifananisha na mchezaji gani wa timu ya United kama Eric Cantona au Zlatan Ibrahimovic, alijibiwa: “Hapana, Kim ni Kim — Yeye yuko peke yake.”
Mtoto wa rais huyo, Han Jwang-song aliangalia mechi kati ya Perugia nchini Italia na kuripotiwa sana kwenye vyombo vya habari.
Razzi alisema Kim alimwambia anaamini katika siku si nyingi wachezaji wa Korea wataanza kung'ara duniani kwa kuwa nchi yake imekuwa katika mapinduzi.
Anaamini wachezaji wa nchi yake watacheza hata katika Ligi Kuu England.
Razzi mtu mwenye nguvu katika siasa za Italia, anajulikana nchini kwake kutokana na urafiki wake na Kim.
Amekuwa akimwalika mara kwa mara nyumbani kwake na kumwelezea yeye na majenerali wake kama watu wanaosisimua.
Kim ni shabiki wa mpira, amewahi kwenda kuangalia mechi San Siro alipokuwa mtoto wakati alipokuwa akisoma Uswisi.
Uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Marekani umeharibika katika siku za karibuni baada ya kuripotiwa Korea Kasikazini kurusha makombola kuelekeza Japan na kufanya majaribio ya silaha za nyukilia katika eneo hilo.
Marekani imekuwa ikiiambia China kusaidia dhidi ya Korea Kaskazini ambayo inaonekana kutaka kuvunja amani katika eneo hilo la Asia.


Comments
Post a Comment