Skip to main content

Phiri aitega Mbeya City kuhusu mkataba


Kocha Kinnah  Phiri (katikati) wakati alipokuwa kazini, akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Mbeya City msimu uliopita.

Mwandishi Wetu
WAKATI klabu ya Mbeya City FC ikisema imefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na mkataba na Mmalawi Kinnah  Phiri, kocha huyo ameibuka amesema mkataba wake haujavunjwa (uko hai), utakuwa utavunjwa baada ya kulipwa fedha zake.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amoss Makalla aliingilia kati na kuwa msuluhisi wa mgogoro kati ya Mbeya City na kocha huyo aliyemwomba kumsaidia kutokana na kutolipwa malimbikizo ya mshahara wake na kutohudumiwa.

Katika taarifa yake, iliyotoka jana Klabu ya Mbeya City FC imesema imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na aliyekuwa kocha wake mkuu, Kinnah F. Phiri

Taarifa kamili ya Mbeya City iliyotolewa jana kwenye tovuti yake na Ofisa na Habari wake Shah Mjanja inasomeka;

Klabu ya Mbeya City FC leo tarehe 13.09.2017 imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na aliyekuwa kocha Mkuu wake Kinnah F. Phiri.

Kikao cha leo ulikuwa ni mwendelezo wa vikao kadhaa baina ya pande hizi mbili toka mwezi Julai mwaka huu. Baada ya majadiliano marefu pande zote mbili zimekubaliana kutoendelea na makubaliano yao ya hapo awali.

Sababu kubwa ni matokeo mabaya ya timu ya msimu uliopita 2016/2017 ambayo yameipunguzia klabu uwezo mkubwa wa kuhimili mahitaji yake ya msingi baada ya wadhamini waliotarajia kuingia kushindikana na wadhamini waliopo kupunguza kiwango cha udhamini wao kutokana na matokeo hayo yasiyoridhisha.

Klabu itatangaza kocha mkuu baada ya muda mfupi ujao ila kwa sasa timu itabaki chini ya usimamizi wa kocha msaidizi, Mohamed Kijuso.

Klabu inapenda kumshukuru Kocha Phiri kwa mchango wake muhimu katika timu yetu, itaendelea kuuthamini na kuukumbuka na inaamini Kocha Phiri ataendelea kuwa msaada katika maendeleo ya timu yetu kwani amekuwa sehemu ya familia yetu.

Hata hivyo akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari jana, Phiri alisema mkataba wake bado uko hai, walikubaliana City itafute kocha wa kusimamia timu kwa muda, mkataba wake utavunjwa pale atakapokuwa amelipwa malimbikizo ya mshahara na stahili zake nyingine ambapo kwa jumla ni takriban sh. milioni 40.
Alisema anataka alipwe fedha hizo, mkataba ukivunjwa ndipo atatafuta timu nyingine ya kuifundisha.
Alisema wamekubaliana  alipwe fedha zake ndani ya kipindi miezi mitatu, kama hatalipwa  yuko tayari kuomba Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) limsaidie kitu ambacho kitafanya City kulipa fedha nyingi zaidi.
Phiri alisaini mkataba wa miaka miwili Februari 8, 2016 akichukua nafasi ya Meja Mstaafu, Abdul Mingange ambaye naye alichukua nafasi hiyo baada ya aliyekuwa kocha mkuu, Juma Mwambusi kuhamia Yanga kuwa kocha msaidizi wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Hans Pluijm ambaye kwa sasa anainoa Singida United.
Sintofahamu ya mkataba huo, imekuja siku chache tangu Phiri agome kukifundisha kikosi cha Mbeya City kwa madai ya malimbikizo ya mshahara, huku Mbeya City wakionekana kutomjali kabisa.
Katika msimu huu, Mbeya City imecheza michezo miwili ambayo yote imeongozwa na Kocha msaidizi Mohammed Kijuso, ina alama 3 baada ya kushinda mchezo mmoja dhidi ya Majimaji na kupoteza dhidi ya Ndanda FC.
Kuvunjwa kwa mkataba huo kunakuja siku chache toka Phiri agome kukifundisha kikosi cha Mbeya City kwa madai ya malimbikizo ya mshahara, huku Mbeya City wakionekana kutomjali kabisa.
Mpaka sasa Mbeya City imecheza michezo miwili ambayo yote Imeongozwa na Kocha msaidizi Mohammed Kijuso.
Katika michezo hiyo Mbeya City wamekusanya alama 3 baada ya kushinda mchezo mmoja dhidi ya Majimaji, na kupoteza dhidi ya Ndanda FC.

Rekodi ya Phiri 
Phiri alijiunga na City Februari 8, 2016 akitokea klabu ya Free State ya Afrika Kusini , ameiongoza City katika michezo 44, akishinda michezo 12, akifungwa 15 na kutoka sare 17, ilifunga mabao 47 na kufungwa 54.
Phiri alijiunga na City Februari 8, 2016 akitokea klabu ya Free State ya Afrika Kusini na ameiongoza Timu hiyo katika michezo 44, akishinda michezo 12, akifungwa 15 na kutoka sare 17 huku akifunga mabao 47 na kufungwa mabao 54.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...