Skip to main content

Okwi azua mjadala Tuzo Mchezaji Bora wa Mwezi

Emmanuel Okwi (wapili kulia) akishangilia na wachezaji wenzie moja ya mabao maane aliyofunga katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting. Simba ilishinda mabao 7-0.

Mwandishi wetu
TUZO aliyopata mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi ya Mchezaji Bora wa Agosti wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018 imezua mjadala miongoni mwa wadau wa mpira wa miguu.

Okwi alitangazwa jana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa ofisa habari wake, Alfred Lucas leo, kuwa ametwaa tuzo hiyo kwa kuchanguliwa na Kamati ya Tuzo ya TFF, kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha wa viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa. 

Baadhi ya wadau baada ya kusikia ametangazwa wameonesha hisia zao katika mitandao ya kijamii na vipindi vya redio vya michezo, baadhi wakihoji imekuwaje amechaguliwa kuwa mchezaji moja wa mwezi kwa kucheza mechi moja ambayo ilikuwa ya ufunguzi wa ligi, huku wengine wakiunga mkono kuwa pamoja na kuwepo mechi moja ndiye alicheza vizuri na kuisaidia timu yake kupata ushindi mnono.
 Hata hivyo katika taarifa yake  TFF, imesema Okwi alishindanishwa na kiungo wa Mtibwa Sugar, Mohammed Issa ambaye alisaidia timu yake kupata pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0 katika mchezo dhidi ya Stand United uliofanyika Uwanja wa Manungu, Turiani, ambapo alikuwa nyota wa mchezo huo. Mwingine aliyeshindana na Okwi ni Boniface Maganga wa Mbao FC.
 Pia Maganga alitoa mchango mkubwa katika ushindi wa ugenini wa bao 1-0, ambao timu yake iliupata dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba ikiwa  ni pamoja na kufunga bao hilo. 
Ushindi wa Okwi unatokana na kutoa mchango mkubwa katika mchezo wa Simba dhidi ya Ruvu Shooting uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 7-0, huku Okwi akifunga mabao manne. 
Pia Okwi amekuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kufunga hat-trick  (mabao matatu katika mchezo mmoja) katika Ligi Kuu ya Vodacom inayoshirikisha timu 16, ambapo hat trick hiyo alifunga ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Mwezi huo ulikuwa na raundi moja tu iliyochezwa Agosti 26 na 27 mwaka huu ambapo kila timu ilicheza mechi moja. 
Kutokana na kutwaa tuzo hiyo, Okwi ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) atazawadiwa kitita cha Sh. 1,000,000 (milioni moja) na Kampuni ya Vodacom Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...