| Emmanuel Okwi akishangilia bao alilofunga. |
Benedict Myonga
MSHAMBULIAJI Emmanuel Okwi amekuwa kinara wa ufungaji mabao akizishinda timu zote za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, akiwa amefunga mabao sita katika mechi mbili.
![]() |
| Emmanuel Okwi (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzie baada ya kufunga moja ya mabao yake. |
Kwa ujumla timu ya Simba, inanolewa na kocha kutoka Cameroon, Joseph Omog ambayo ni ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi saba sawa na Azam iliyopo katika nafasi ya tatu, ina mabao 10 na haijafungwa huku sita kati ya hayo yamefungwa na Okwi ambaye amesainiwa na Simba kwa mara ya tatu.
Idadi ya mabao aliyofunga Okwi yanazishinda timu zote 15 za Ligi Kuu, ikiwemo vinara Mtibwa Sugar wenye pointi tisa ambao kwa jumla wamefunga mabao 4 na kufungwa moja, Azam yenye mabao mawili, Singida United yenye pointi sita, iliyofunga manne na kufungwa matatu, Mbeya City iliyofunga mabao mawili na kufunga moja.
Pia Okwi anazishinda Tanzania Prisons (4), Yanga (3), Lipuli FC (2) zenye pointi tano kila moja huku na Ndanda iliyo na pointi nne imefunga bao moja na Mbao FC inakamilisha 10 bora ikiwa na mabao matatu.
Timu nyingine na idadi ya mabao iliyofunga katika mabano ni Mwadui (2),
Majimaji (3), Ruvu Shooting (1), Kagera Sugar(1), Njombe Mji (1)na Stand United (0).
Ufuatao ni msimamo kamili wa Ligi Kuu Tanzania baada ya kuisha meshi za mwishoni mwa wiki.
Msimamo Ligi Kuu Vodacom Tanzania 2017
Na Timu P W D L GF GA GD PTS
1 Mtibwa Sugar 3 3 0 0 4 1 3 9
2 Simba SC 3 2 1 0 10 0 10 7
3 Azam FC 3 2 1 0 2 0 2 7
4 Singida United 3 2 0 1 4 3 1 6
5 Mbeya City 3 2 0 1 2 1 1 6
6 Tanzania Prisons 3 1 2 0 4 3 1 5
7 Yanga 3 1 2 0 3 2 1 5
8 Lipuli FC 3 1 2 0 2 1 1 5
9 Ndanda 3 1 1 1 1 1 0 4
10 Mbao FC 3 1 0 2 3 4 -1 3
11 Mwadui 3 1 0 2 2 5 -3 3
12 Majimaji 3 0 2 1 3 4 -1 2
13 Ruvu Shooting 3 0 2 1 1 8 -7 2
14 Kagera Sugar 3 0 1 2 1 3 -2 1
15 Njombe Mji 3 0 0 3 1 4 -3 0
16 Stand United 3 0 0 3 0 3 -3 0

Comments
Post a Comment