Skip to main content

Neymar aeleza ameipendea nini PSG, atabiri neema Ligi ya Mabingwa

Neymar akionesha jezi yake siku alipotambulishwa PSG akitokea Barcelona ya Hispania.
GLASGOW, Scotland
NEYMAR Santos amesisitiza amehama  Barcelona  kwenda Paris kwa matumaini ya kupata mafanikio kwenye Ligi ya Mabingwa.
Paris Saint-Germain katika dirisha la usajili lililopita imevunja rekodi ya Dunia kwa kumsajili nyota huyo wa Brazil kwa ada ya pauni  milioni 198 (zaidi ya sh. bilioni 598 na kumnyakua kutoka Uwanja wa Nou Camp, ikivunja mkataba wake.
Neymar anayepata kiasi cha pauni 500,000 kwa wiki amesema sababu kubwa iliyofanya ahamie PSG ni kutokana na kuona ina nafasi ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa.
Akiwa na  Barcelona Neymar alitwaa mataji nane katika misimu minne akicheza pamoja na Lionel Messi na Luis Suarez katika sehemu ya ushambuliaji.
Leo atacheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya mabingwa awakiwa na PSG dhidi ya Celtic  katika Uwanja wa Parkhead.

Neymar akifurahia moja ya bao alilofunga wakati alipokuwa  Barcelona.

Neymar (25), alisema: “moja ya sababu kubwa ya kujiunga na PSG ni kusaidia kuandika historia. Ligi ya Mabingwa, si tu taji tunalolitaka kuchukua, lakini taji muhimu sana.
“Lengo la msimu huu ni kujaribu kutwaa, hilo ni daraja ambalo kwa sasa klabu ipo. Ninaamini tunauwezo wa kutwaa ubingwa.
“Si tu kwamba tukwamba tuna ubora lakini tuna uzoefu, wachezaji ambao wanajua kitu gani cha kufanya ili kutwaa Ligi ya Mabingwa.
“Nimeshatwaa ubingwa wa mashindano hayo, Dani Alves ametwaa mara tatu, Thiago Motta ametwaa ubingwa akiwa na Barcelona na Inter, Angel Di Maria alitwaa ubingwa Real Madrid.  Si tu tuna ubora, lakini uzoefu wa kweli.”
Kuhusu ada yake aliyolipiwa alisema yeye hahusiki na lolote,  ni klabu zenyewe zilizokubaliana.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...