![]() |
| Wayne Rooney , Coleen wakati wa furaha |
LONDON, Uingereza
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amewaambia rafiki zake anahofia ndoa yake itavunjika baada ya mkewe Coleen kuwachukua watoto wao watatu na kuondoka nao.
Coleen (31) ambaye ni mjamzito wikiendi hii alipumzika na wazazi wake, baada ya Rooney kukamatwa na polisi na kushikiliwa kwa muda kutokana na kuendesha gari huku akiwa amelewa na alikuwa na mwanamke mwingine (mchepuko) aitwaye Laura Simpson.
Coleen, aliondoka kwenye nyumba yao na Rooney Jumamosi mchana na kuwasili kwenye nyumba ya familia yao akiwa na gari aina ya Range Rover akiwa na watoto wake wa kiume Kai (7), Klay (4) Kit mwenye mwaka mmoja.
Aliondoa kwenye nyumba yao saa chache baada ya kurejea kutoka Majorca, Hispania mapumzikoni na kujua kuwa mumewe ambaye ni mshambuliaji wa Everton alitiwa mbaroni kwa kuendesha gari huku akiwa amelewa na kwenye gari lake alikuwa na mchepuko Laura Simpson (29) ambaye ni mmoja wa wanawake wenye tabia ya kwenda kwenye klabu za starehe mara kwa mara.
Chanzo kimesema: “ Coleen ameamua kukaa na wazazi wake wakati akipanga ni kitu gani cha kufanya, lakini kwa wakati huu anahisi ndoa yake na Rooney ya miaka tisa itakuwa imeisha.
“Mambo yanaweza kubadilika katika siku zijazo lakini kwa sasa anaona inatosha na imekwisha. Anahisi kudhalilishwa. Anapanga kuondoka.”
Habari nyingine zinadai kuwa Wayne (31) amewaambia rafiki zake anahofia ndoa yake ya miaka tisa imekwisha. Hajui afanye nini.
“Alishaomba radhi kwa Coleen kwa mambo mengi aliyofanya nyuma, lakini bado inaonekana kuwa ngumu. Amechanganyikiwa.”
Coleen alisema jana kuwa ataendelea kubakia na watoto wake kama yeye na Rooney watatengana.
Ameweka kwenye kwenye mtandao wake wa Instagramn picha ya watoto wake na kuandika: “Bila ya kujali niko wapi kila wakati watanifuata na ninatumaini itakuwa hivyo.”
Wazazi wa Coleen wamekataa kuzungumza na mkwe wao Rooney ambaye ni nahodha wazamani wa England .
Rafiki wa karibu wa Rooney na ndugu zake nao hawajaonekana kuwa karibu naye.
![]() |
| Nyumba ya Rooney na mkewe Coleen. |
Coleen akiwa na Colette walikwenda nyumbani kwa Rooney, Prestbury, Cheshire Ijumaa na Coleen alimcharukia Wayne kuwasili akikatisha mapumziko yake nchini Hispania baada ya kusikia kukamatwa kwa mumewe.
Awali wiki mbili zilizopita Coleen aliweka picha yake inamwonesha akiwa na Rooney katika Instagram baada ya mume wake kutangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa ya England.
Aliandika chini yake: “Hongera kwa uchezaji wa kusisimua England! Tunakupenda na tunajivunia sana wewe !”
Wayne na mchepuko Laura walikutana Alhamisi usiku katika baa ya Symposium, Wilmslow kisha walichukua taksi iliyowapeleka mahali alikopaki gari, kabla ya kuendesha umbali wa km 21 kuelekea nyumbani kwake.
Laura amesema hakuna kitu kibaya alichofanya na nyota huyo.
Wakala wa Wayne, Paul Stretford aliwasili kwenye nyumba ya nyota huyo kuzungumza naye.
![]() |
| Laura Simpson |
Mwaka 2010 wakati Coleen alipokuwa na ujauzito wa Kai, Wayne alidaiwa kufanya mapenzi na Jenny Thompson na Helen Wood ambao nao ni wanawake wanaojirusha kwenye klabu za starehe
Wayne anatakiwa kufika kwenye mahakama ya Stockport Septemba18 kujibu mashtaka ya kuendesha gari huku akiwa amelewa.
Kocha wake katika timu ya Everton manager Ronald Koeman leo anatarajiwa kuzungumza naye. Anaweza kutozwa faini ya mshahara wa wiki mbili kiasi cha pauni 320,000 (zaidi ya sh milioni 928.



Comments
Post a Comment