![]() |
| Rafael Nadal |
NEW YORK, Marekani
RAFAEL Nadal ametwaa ubingwa wa mashindano ya Wazi ya Marekani kwa mara ya tatu na taji lake la 16 katika mashindano makubwa ya kila mwaka 'Grand Slam' baada ya kumshinda Kevin Anderson wa Afrika Kusini katika mchezo wa fainali uliochezwa New York alifajili ya leo.
Mchezaji huyo namba moja kwa ubora duniani alishinda kwa seti 3-0, akipata alama 6-3 6-3 6-4 katika Uwanja wa Flushing Meadows.
Pamoja na kutwaa taji hilo, Nadal amepata zawadi ya fedha kiasi cha dola 3,700,000 ambazo ni sawa na sh. bilioni 8.4 za Tanzania huku mpinzani wake akipata bilioni 4.2 na kombe dogo.
Nadal mwenye umri wa miaka (31), kwa mwaka huu ametwaa mataji mawili ya Slam kwa mwaka mmoja ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 2013, taji jingine la mwaka huu alitwaa katika mashindano ya Ufaransa.
Safari ya Nadali kabla ya kutwaa ubingwa wa tenisi Marekani mwaka huu ilikuwa kama ifuatavyo;
Mzunguko wa kwanza: Alimfunga Dusan Lajovic (Serbia) 7-6 (7-6) 6-2 6-2
Mzunguko wa pili: Alimfunga Taro Daniel (Japan) 4-6 6-3 6-2 6-2
Mzunguko wa tatu : Alimfunga Leonardo Mayer (Argentina) 6-7 (7-3) 6-3 6-1 6-4
Mzunguko wa nne: Alimfunga Alexandr Dolgopolov (Ukraine) 6-2 6-4 6-1
Robo fainali: Alimfunga Andrey Rublev (Russia) 6-1 6-2 6-2
Nusu Fainali: Alimfunga Juan Martin del Potro (Argentina) 4-6 6-0 6-3 6-2
Fainali: Alimfunga Kevin Anderson (Afrika Kusini) 6-3 6-3 6-4

Comments
Post a Comment