Mwandishi wetu
WAKATI timu ya Mtibwa Sugar ikiilaza Mbao kwa mabao 2-1 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu ya Vodacom kwa kufikisha pointi tisa ikishinda mechi zake zote tatu za kwanza, Majimaji na Yanga zimegawana pointi kwa kufungana bao 1-1.
Bao lililofungwa na Donald Ngoma dakika ya 79 kwa kichwa akiunganisha krosi ya Obrey Chirwa liliwanusuru mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Yanga kupoteza mchezo dhidi ya wenyeji wao Majimaji katika mchezo wa mzunguko wa tatu uliopigwa mjini Songea .
Majimaji ilianz akupata bao dakika ya 54, likifungwa na Peter Mapunda kwa shuti la mguu wa kushoto akitumi vema p pasi ya Marcel Kahenza.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi tano huku na kupanda hadi nafasi ya tatu huku Majimaji ikifikisha pointi mbili katika michezo mitatu.
Katika mchi zao zijazo Yanga itapam,bana na Ndanda Septemba 23 mwaka huu Uwanja wa Uhuru huku Majimaji itakuwa nyumbani tena kuchuana na Mji Njombe
Matokeo ya mechi nyingine, Prisons ilitoka suluhu dhidi ya Ndanda, Singida United ilishinda bao 1-0 dhidi ya Stand United, Lipuli FC ilitoka sulugu dhidi ya Ruvu Shooting.

Comments
Post a Comment