![]() |
| Jose Mourinho (kushoto) na Arsene Wenger . |
LONDON, Uingereza
JOSE Mourinho amesema anawasikitikia mashabiki wa Arsenal na kuongeza kuwa hajui ni kwa nini Arsene Wenger anaendelea kuiongoza timu yao, kwa mujibu wa Piers Morgan.
Mourinho alimpiga kijembe hasimu wake huyo katika Ligi Kuu baada ya kukutana na Morgan ambaye ni mwanzisdhi wa habari na shabiki wa Arsenal wakati alipomaliza kufanya manunuzi katika duka la Harrods.
![]() |
| Arsene Wenger (kushoto) akisukumana na Jose Mourinho katika moja ya mechi zilizokutanisha timu zao. |
Gunners imeanza msimu wa Ligi Kuu England mpya vibaya kwa kupoteza mechi mbili, huku Manchester United ikipewa nafasi kutwaa ubingwa baada ya kuanza msimu wa 2017/18 vizuri na kwa sasa inaongoza Ligi kwa kuwa na pointi ikiwa na pointi 10 sawa na mahasimu wao Manchester City baada ya kushinda mechi tatu na kutoka sare moja.
Makocha hao wamekuwa na upinzani, Mourinho amekuwa na tabia ya kumtania Wenger kuna wakati Wenger alimsukuma Mourinho alipokwenda kushangilia na kutoa maelekezo kwa timu yake katika eneo lisilostahili kwake.
Katika kijembe cha safari hii Mourinho amedai mashabiki wa Arsenal wamekuwa na msongo wa mawazo kutokana na matokeo mabaya ya timu yao na anashangaa ni kwanini hadi sasa bado inanolewa na Wenger.


Comments
Post a Comment