![]() |
| Mshambuliaji wa Liverpool na Misri, Mohamed Salah (wapili kushoto) akisepa na kijiji cha wachezaji wa Uganda katika mchezo uliofanyika mjini Alexandria, Misri jana. Misri ilishinsda bao 1-0. |
CAIRO, Misri
MSHAMBULIAJI wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah amefunga bao pekee dhidi ya Uganda, ambalo limefufua matumaini ya timu yake kufuzu fainali za kombe la Dunia 2018.
Kwa matokeo hayo Uganda italazimika kupambana kupata ushindi katika michezo miwili iliyobaki na kuombea Misri ipoteze kuweza kufuzu fainali hizo.
Misri ambayo haijafuzu fainali za Kombe la Dunia tangu mwaka 1990 inaongoza kundi E sasa ina pointi tisa, huku Uganda ambayo nayo wiki mbili zilizopita iliifunga Misri bao 1-0 lililofungwa na Emmanuel Okwi imebaki na pointi saba.
Nyota wa Liverpool, Salah alifunga bao hilo dakika ya sita baada ya Abdallah Said kupifa shuti na kuokolewa mlinda mlango Denis Onyango na mpira kumkuta mfungaji alioukwamisha wavuni.
Onyango baadaye aliokoa mpira uliopigwa na Said na Ramadan Sobhi na kuinyima nafasi Misri kupata bao la pili, huku safu ya ushambuliaji ya Uganda ikishindwa kuipenya ngome ya Misri iliyokuwa chini ya mlinga mlango mkongwe Essam El Hadary mwenye umri wa miaka 44.
Kocha wa Misri raia wa Argentina, Hector Cuper anaweza kuivusha timu hiyo kwenda fainali za Kombe la Dunia kama atashinda mechi bili zilizosalia, mchezo wa nyumbani dhidi ya
Congo wa Oktoba 8 kwenda kucheza ugenini dhidi ya Ghana mchezo wa mwisho Novemba.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, Ghana iliichapa Congo mabao 5-1 matokeo ambayo umafanya ifikishe pointi tano na kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo na Congo kuwa ya mwisho ikiwa na pointi moja huku ikiondoka katika mbio za kufuzu fainali hizo zitakazofanyika Urusi.
Uganda katika mechi zake mbili za mwisho itacheza dhidi ya Ghana Oktoba 7 kabla ya kwenda kwenda Congo kumalizia mchezo wa mwisho Novemba.
Matokeo mengine ya mechi zilizofanyika jana ni kama ifuatavyo;
Afrika Kusini 1 - 2 Cape Verde
Congo DR 2 - 2 Tunisia
Ivory Coast 1 - 2 Gabon
Burkina Faso 2 - 2 Senegal
Mali 0 - 0 Morocco
Algeria 0 - 1 Zambia
ZINGATIO: Timu itakayoongoza kila kundi baada ya kuchezwa mechi za mwisho itakuwa imefuzu michuano hiyo itakayofanyika Urusi.
MSIMAMO WA MAKUNDI AFRIKA KUWANIA KUFUZU kOMBE LA DUNIA 2018.
KUNDI A
| P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts | |||
| 1 | Tunisia | 4 | 3 | 1 | 0 | 7 | 3 | 4 | 10 | ||
| 2 | DR Congo | 4 | 2 | 1 | 1 | 9 | 5 | 4 | 7 | ||
| 3 | Guinea | 4 | 1 | 0 | 3 | 4 | 7 | -3 | 3 | ||
| 4 | Libya | 4 | 1 | 0 | 3 | 3 | 8 | -5 | 3 |
KUNDI B
| P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts | |||
| 1 | Nigeria | 4 | 3 | 1 | 0 | 10 | 3 | 7 | 10 | ||
| 2 | Zambia | 4 | 2 | 1 | 1 | 6 | 4 | 2 | 7 | ||
| 3 | Cameroon | 4 | 0 | 3 | 1 | 3 | 7 | -4 | 3 | ||
| 4 | Algeria | 4 | 0 | 1 | 3 | 3 | 8 | -5 | 1 |
KUNDI C
| P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts | |||
| 1 | Cote d'Ivoire | 4 | 2 | 1 | 1 | 7 | 3 | 4 | 7 | ||
| 2 | Morocco | 4 | 1 | 3 | 0 | 6 | 0 | 6 | 6 | ||
| 3 | Gabon | 4 | 1 | 2 | 1 | 2 | 4 | -2 | 5 | ||
| 4 | Mali | 4 | 0 | 2 | 2 | 1 | 9 | -8 | 2 |
KUNDI D
| P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts | |||
| 1 | Burkina Faso | 4 | 1 | 3 | 0 | 5 | 3 | 2 | 6 | ||
| 2 | Cape Verde | 4 | 2 | 0 | 2 | 4 | 6 | -2 | 6 | ||
| 3 | Senegal | 4 | 1 | 2 | 1 | 5 | 4 | 1 | 5 | ||
| 4 | Africa Kusini | 4 | 1 | 1 | 2 | 5 | 6 | -1 | 4 |
KUNDI E
| Na | Timu | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
| 1 | Misri | 4 | 3 | 0 | 1 | 5 | 2 | 3 | 9 |
| 2 | Uganda | 4 | 2 | 1 | 1 | 2 | 1 | 1 | 7 |
| 3 | Ghana | 4 | 1 | 2 | 1 | 6 | 4 | 2 | 5 |
| 4 | Congo | 4 | 0 | 1 | 3 | 3 | 9 | -6 | 1 |

Comments
Post a Comment