![]() |
| Conor McGregor (watatu kushoto) akiwa na rafiki zake na familia yake katika kisiwa cha Ibiza Hispania leo. |
MADRID, Hispania
BONDIA Conor McGregor ameamua kusahau kipigo alichopata kutoka wa Floyd Mayweather mjini Las Vegas wiki mbili zilizopita kiasi cha kufanya mwamuzi akatishe pambano katika raundi ya 10 katika Ukumbi wa T-Mobile Arena, kwa kwenda mapumziko au kula bara kwenye kisiwa cha Ibiza, Hispania.
McGregor ameonekana akiwa amelala kwenye jua, akiwa na familia yake na rafiki zake.
Akiwa katika kisiwa hicho, bondia huyo alionekana akiendesha pikipiki kwenye maji na kula na kunywa kwenye boti ya kifahari akiwa na watu wake wa karibu.
Nyota huyo akwia ibiza amekodi nyumba kwa wiki moja kwa ajili ya rafiki yake ambaye amefunga ndoa.
![]() |
| McGregor akiwa amembeba mwanaye. |
Ameripotiwa kuingia fedha kiasi cha pauni 100 (zaidi ya sh. bilioni 29) kwa kupigana na Mayweather mwezi uliopita McGregor kwa sasa hana haraka ya kurudi tena kazini (kupigana), kocha wake John Kavanagh amesema huenda asipande ulingoni hadi mwaka 2018.
Nyota huyo mwenye umri wamiaka 29 anatarajiwa kurejea ulingoni na kucheza mchezo aliouzoea wa ngumi mchanganyiko,huku Nate Diaz akipewa na nafazi ya kuwa mpinzani wake.




Comments
Post a Comment