![]() |
| Floyd Mayweather (kulia) akimtwanga konde Conor McGregor, |
LAS VEGAS, Marekani
BONDIA Floyd Mayweather alijaribu kutaka kubashiri matokeo ya pambano la ngumi kati yake na Conor McGregor kwa pauni 310,00 (zaidi ya sh. milioni 899) kabla ya kuamua kuacha.
Mayweather amekuwa na tabia ya kupenda kubeti hasa kunapokuwa na mechi za mpira wa kikapu na mara nyingi amepata, aliamua kuacha kwa kuhofia kubabwa na sheria, kutabiri matokeo huku yeyer mwenyewe akiwa mchezaji.
Kitu kingine kilichofanya aachane na kucheza, ni kutokana na wachezaji kuchelewa kukamilisha tararibu.
![]() |
| Floyd Mayweather akionesha fedha katika moja ya tambo zake kuonesha anamiliki kiasi kikubwa cha fedha. |
Hata hiyo kwa kucheza pambano hilo ambalo alishinda dhidi ya McGregor mjini Las Vegas, Marekani alipata fedha zaidi ya pauni milioni 77.6 (zaidi ya sh. bilioni 223).
Kama angebashiri matokeo hayo na kupatia angeweza kupata pauni milioni 271( zaidi ya sh. bilioni 786).
Kwa mujibu wa ESPN, Mayweather aliwasiliana na mchezeshaji bahati nasimu wa Las Vegas saa moja kabla ya kupanda ulingoni, akitaka kuwe pauni 310,000 katika pambano lake lilichezwa kwa raunfi tisa na nusu.


Comments
Post a Comment