Skip to main content

Mayweather adai kuwa na wapenzi saba, magari 25


Floyd Mayweather akisikiliza swali kutoka  kwa Awkward Puppets.

NEW YORK, Marekani
BONDIA  Floyd Mayweather amesema kuwa anawapenzi saba kwa kuwa anaona kuwa na mmoja na ni sawa na kukaribia kutokuwa naye.

Baadhi ya magari yanayomilikiwa na  Floyd Mayweather.

Mbabe huyo wa ngumu alisema hayo wakati akijibu swali la mtangazaji Diego lilikuwa likiulizwa ana kinyago kiitwacho Awkward Puppets, cha  YouTube, mambo mengine aliyohojiwa ni kiasi gani cha fedha alizonazo benki.

Katika mahojiano, Mayweather alisema ana wapenzi wanawake saba na anamiliki magari ya kifahari 25 yaliyoko Las Vegas ,lipo Bugatti jekundu na  Ferrari yan njano.
Mayweather pia amesema fedha alizopata katika pambano lake la mwisho dhidi ya Conor McGregor mwezi uliopita ni za mwisho kulizpatia ulingoni.



'' Pambano la mwisho ni lile nilikocheza, lile lilikuwa ni pambano la fedha,' Mayweather  alisema na kuongeza  anajua kuna watu watataka kupigana naye tena katika sayari nyingine.



Mayweather alifanya mahojiano hayo na Diego katika klabu yake ya usiku iliyopo Las Vegas, iitwayo Girl Collection (Mkusanyiko wa wanawake).
Alipoulizwa ana wanawake wangapi alijibu yeye si mwanaume mwaminifu wa kuwa na mwanamke mmoja.



''Nina wanawake wangapi? Pengine kama saba,'' Mayweather alisema. 
'' Tunakwenda kula pamoja, baadhi husafiri pamoja. Kuwa na mmoja ni sawa na karibu kutokuwa naye.'' 
Kuhusu fedha, Mayweather alisema na fedha nyingi katika akaunti zake benki, zinaweza kuwa dola milioni 200 hadi milioni 300.
Mayweather anakadiriwa kupata dola milioni 100 katika pambano lake dhidi ya McGregor Agosti mwaka huu.
Alimtwanga kwa TKO katika raundi ya 10 na kumfanya mwamuziki kusimamisha pambano, hivyo kureka rekodi ya kushinda mapambano 50 bila ya kupigwa. 

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...