![]() |
| Wachezaji wa Manchester United wakishangilia moja ya mabao yao dhidi ya Everton jana. |
LONDON, Uingereza
USHINDI wa mabao 4-0 iliopata Manchester United dhidi ya Everton katika Uwanja wa Old Trafford umeongeza presha dhidi ya Manchester City kileleni ambapo kwa sasa timu hizo ziko sawa kwa kila kitu.
Katika mchezo dhidi ya Everton, United ilifunga mabao matatu katika dakika sita za mwisho na kufanya kocha Ronald Koeman kuendelea kuwa kwenye presha ikiwa nafasi ya 18 kwenye msimamo na kuwa na pointi nne katika michezo mitano.
![]() |
| Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero akishangilia baada ya kufunga bao kwenye mchezo dhidi ya Watford. |
Antonio Valencia alifunga bao la kuongoza dakika ya nne kabla ya Henrikh Mkhitaryan, Romelu Lukaku na Anthony Martial (penalti) kufunga katika dakika sita za mwisho.
Awali Manchester City Jumamosi ilishinda mabao 6-0 ugenini dhidi ya Watford ikiwa ni kipigo cha pili mfululizo baada ya kuifunga Liverpool mabao 5-0 katika Uwanja wa Etihad.
City inayonolewa na Kocha Pep Guardiola hadi sasa ina pointi 13, imecheza mechi tano, imeshinda nne, sare moja , moja na haijapoteza, imefunga mabao 16 kufungwa mawili, tofauti ya mabao ni 14, iko sawa kila kitu na United ambayo ni hasimu wake katika mji mmoja.
Everton, baada ya kufungwa mabao 4-0 dhidi ya United, inakuwa imefungwa mabao 12 katika mechi nne za mwisho za mashindano yote na kushindwa kufunga bao.
Timu hiyo imetumia pauni milioni 140 katika majira ya joto yaliopita kwa usajili, ilijiwekea malengo ya kumaliza katika timu nne za juu, kitu ambacho kinaonekana kinaweza kuwa kigumu kwa mwenendo wake wa sasa.
Ufuatao ni msimamo wa Ligi Kuu England baada ya mechi za mwishoni mwa wiki.
Msimamo Ligi Kuu England 2017/2018
| Na | Timu | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
| 1 | Manchester City | 5 | 4 | 1 | 0 | 16 | 2 | 14 | 13 |
| 2 | Manchester United | 5 | 4 | 1 | 0 | 16 | 2 | 14 | 13 |
| 3 | Chelsea | 5 | 3 | 1 | 1 | 8 | 5 | 3 | 10 |
| 4 | Newcastle United | 5 | 3 | 0 | 2 | 6 | 4 | 2 | 9 |
| 5 | Tottenham Hotspur | 5 | 2 | 2 | 1 | 7 | 3 | 4 | 8 |
| 6 | Huddersfield Town | 5 | 2 | 2 | 1 | 5 | 3 | 2 | 8 |
| 7 | Burnley | 5 | 2 | 2 | 1 | 6 | 5 | 1 | 8 |
| 8 | Liverpool | 5 | 2 | 2 | 1 | 9 | 9 | 0 | 8 |
| 9 | Southampton | 5 | 2 | 2 | 1 | 4 | 4 | 0 | 8 |
| 10 | West Bromwich Albion | 5 | 2 | 2 | 1 | 4 | 4 | 0 | 8 |
| 11 | Watford | 5 | 2 | 2 | 1 | 7 | 9 | -2 | 8 |
| 12 | Arsenal | 5 | 2 | 1 | 2 | 7 | 8 | -1 | 7 |
| 13 | Stoke City | 5 | 1 | 2 | 2 | 5 | 6 | -1 | 5 |
| 14 | Swansea City | 5 | 1 | 2 | 2 | 2 | 5 | -3 | 5 |
| 15 | Leicester City | 5 | 1 | 1 | 3 | 7 | 9 | -2 | 4 |
| 16 | Brighton & Hove Albion | 5 | 1 | 1 | 3 | 4 | 7 | -3 | 4 |
| 17 | West Ham United | 5 | 1 | 1 | 3 | 4 | 10 | -6 | 4 |
| 18 | Everton | 5 | 1 | 1 | 3 | 2 | 10 | -8 | 4 |
| 19 | AFC Bournemouth | 5 | 1 | 0 | 4 | 3 | 9 | -6 | 3 |
| 20 | Crystal Palace | 5 | 0 | 0 | 5 | 0 | 8 | -8 | 0 |


Comments
Post a Comment