Skip to main content

Man City fowadi yake moto, yafunga mabao 16 mechi tano * Pata msimamo, ratiba mechi za leo


Wachezaji wa Man City walishangilia moja kati ya mabao 6-0 waliofunga dhidi ya Watford jana.

LONDON, Uingereza
TIMU ya Manchester City baada ya kuifunga Liverpool mabao 5-0, imeonesha kuwa ni moto wa kuotea mbali kwa kuifunga Watford na  mabao 6-0. na kuzidi kuongoza ligi kwa kufikisha pointi 13 baada ya kucheza mechi tano.

 City inayonolewa na kocha Pep Guardiola ikicheza ugenini na ilipata mabao yake matatu kupitia kwa Sergio Aguero (dk. 27' dk. 31' dk. 81' ), Jesus (dk 37), Otamendi (dk.63) na Sterling (dk.89'  pen).

Liverpool ikicheza nyumbani kwenye uwanja wake wa Anfied ilishindwa kutamba na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Burnley.

Matokeo ya mechi nyingine jana yalikuwa

Crystal Palace 0 Southampton 1
Huddersfield Town 1 Leicester City 1
Newcastle United 2 Stoke City 1
West Bromwich Albion 0 West Ham United 0

Man City kwa sasa inaonekana kwua ndiyo timu yake fowadi kali zaidi katika Ligi Kuu England ikiwa imefunga jumla ya mabao 16 na kufungwa mawili katika mechi tano na kujikusanyia pointi 13.

Sergio Aguero ndite anaongoza  katika Ligi Kuu England kwa kugunga mabao matano akifuatiwa na mwchezaji mwenzie kwenye timu moja Jesus mwenye mabao manRomelu Lukaku wa Man united na J. Vardy wa Leicester.
Sadio Mané wa Liverpool na Álvaro Morata wa Chelsea kila mmoja ana mabao mawili. 

Timu inayofuatia ni Man United United ambayo ina pointi 10, lakini imecheza mechi nne na leo inapambana na Everton huku yenyewe ikiwa imefunga sita.

Timu inayoonekana kuwa na safu mbovu zaidi ya ulinzi hadi sasa ni West Ham United ambayo imefungwa mabao 10 na kufunga manne.

Ratiba za mechi za leo

Jumapili Septemba 17, 2017
Chelsea v Arsenal Stamford Bridge        saa 09:30
Manchester United v Everton Old Trafford     saa 12:00



Msimamo Ligi Kuu England
Na Timu                         P W D L GF GA GD Pts
1 Manchester City         5 4 1 0 16 2 14 13
2 Manchester United         4 3 1 0 12 2 10 10
3 Chelsea                         4 3 0 1 8 5 3 9
4 Newcastle United         5 3 0 2 6 4 2 9
5 Tottenham Hotspur         5 2 2 1 7 3 4 8
6 Huddersfield Town         5 2 2 1 5 3 2 8
7 Burnley                         5 2 2 1 6 5 1 8
8 Liverpool                         5 2 2 1 9 9 0 8
9 Southampton                 5 2 2 1 4 4 0 8
10 West Bromwich         5 2 2 1 4 4 0 8
11 Watford                         5 2 2 1 7 9 -2 8
12 Arsenal                         4 2 0 2 7 8 -1 6
13 Stoke City                         5 1 2 2 5 6 -1 5
14 Swansea City                 5 1 2 2 2 5 -3 5
15 Leicester City                 5 1 1 3 7 9 -2 4
16 Brighton                         5 1 1 3 4 7 -3 4
17 Everton                         4 1 1 2 2 6 -4 4
18 West Ham United         5 1 1 3 4 10 -6 4
19 AFC Bournemouth         5 1 0 4 3 9 -6 3
20 Crystal Palace                 5 0 0 5 0 8 -8 0

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...