Skip to main content

Majimaji , Yanga Mtibwa hapatoshi leo, Azam yaongoza Ligi Kuu


Kikosi cha Yanga

Mwandishi Wetu

WAKATI timu ya Azam FC ikiongoza Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 7 baada ya kuifunga Kagera Sugar bao 1-0 Uwanja wa Azam Complex jana, ligi hiyo inaendelea leo.
Bao pekee la Azam FC lilifungwa na Mbaraka Yusuf.
Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa kuzikutanisha timu 10 kwenye viwanja vitano tofauti,  mchezo kati ya Yanga ambayo ni mgeni wa  Majimaji FC ya Songea katika Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma, ukiwa kivutio kwa mashabiki.

Majimaji ambayo ina pointi moja iliyopata wiki ilipita baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Tanzania Prisons baada ya kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza na Mbeya City inapambana na mabingwa watetezi Yanga.
Yanga ina pointi nne baada ya kushinda  ugenini dhidi ya Njombe Mji bao 1-0 wiki iliyopita, baada kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Lipuli FC katika fungua dimba.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa na kuvuta mashabiki wataofika uwanjani na wengine wa mbali watakaoufutilia kwenye runinga.
Majimaji ambayo imekuwa na kawaida ya kucheza kwa ushindani dhidi ya Yanga inapokuwa kwao, itataka kushinda ili kuondoka kwenye nafasi za chini kwenye msimamo, huku Yanga nayo ikitaka kushinda ili kupanda juu kwenye msimamo kutoka nafasi ya nne.
Yanga iliwasili Songea juzi huku meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh akisema wachezaji wote waliosafiri na timu  hiyo wako fiti akiwamo Obrey Chirwa aliyekuwa majeruhi.
Alisema lengo lao ni kupata pointi tatu ingawa wanaamini utakuwa ni mgumu, kwa kuwa timu pinzani zinaonekana kuikamia timu yao, zikifahamu inatetea ubingwa baada ya kutwaa ubingwa mara tatu mfululizo.
Katika mchezo wa leo, Yanga itawakosa, Amiss Tambwe, Beno Kakolanya na Akilimali ambao hawakusafiri na timu kutokana na umajeruhi na kuugua.
Katika mechi nyingine leo Mbao FC yenye pointi tatu ilizopata kwa kushinda mechi moja na kupoteza moja itakuwa Manungu mkoani Morogoro kucheza na vinara katika msimamo Mtibwa Sugar  yenye pointi sita baada ya kushinda mechi zake mbili za mwanzo.
Msimu uliopita katika mchezo wa kwanzo Mbao iliifunga mtibwa mabao 5-0 na katika marudiano zilitoka sare ya bao 1-1. Mchezo wa leo pia unatarajiwa kuwa na ushindani kati ya timu hizo.
Tanzania Prisons ya Mbeya ambayo  iliyotoka sare ya mabao 2-2 na Majimaji wiki iliyopita na kufikisha pointi nne itakuwa tena nyumbani Uwanja wa Sokoine kupambana na Ndanda FC yenye alama tatu.

Lipuli FC iliyoona ushindi wa kwanza katika ligi hiyo kwa kuifunga Stand United bao 1-0 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga, itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Samora, ambayo ina pointi moja iliyopata kwa kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Kagera Sugar na kufungwa bao 7-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa kwanza.
 Singida United  inayonolewa na Kocha wa zamani wa Yanga, Hans Pluijm itawakuwa ni wageni wa Stand United katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga timu hizo kila moja ina pointi tatu baada ya kushinda mechi moja na kufungwa moja.
Kesho kutapigwa mechi mbili, Simba yenye pointi nne itaikaribisha Mwadui yenye pointi tatu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na Mbeya City yenye pointi tatu itaialika Uwanja wa Sokoine, Njombe Mji ambayo haina pointi baada kufungwa mechi mbili za kwanza .


Msimamo Ligi Kuu Tanzania Bara
Na Timu P W D L GF GA GD PTS
1 Azam FC 3 2 1 0 2 0 2 7
2 Mtibwa Sugar 2 2 0 0 2 0 2 6
3 Simba 2 1 1 0 7 0 7 4
4  Prisons      2 1 1 0 4 3 1 4
5 Lipuli FC 2 1 1 0 2 1 1 4
6 Yanga 2 1 1 0 2 1 1 4
7 Singida Utd 2 1 0 1 3 3 0 3
8 Mbao FC 2 1 0 1 2 2 0 3
9 Mwadui 2 1 0 1 2 2 0 3
10 Mbeya City 2 1 0 1 1 1 0 3
11 Ndanda FC 2 1 0 1 1 1 0 3
12 Majimaji FC 2 0 1 1 2 3 -1 1
13 Kagera Sugar 3 0 1 2 1 3 -2 1
14 Ruvu Shooting 2 0 1 1 1 8 -7 1
15 Njombe Mji 2 0 0 2 1 3 -2 0
16 Stand United 2 0 0 2 0 2 -2 0

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...