Skip to main content

Madonna anunua jumba Ureno kumsapoti mwanaye mwanasoka timu ya Benfica


Nyumba aliyoinunua Madonna.

LISBON, Ureno
MWANAMUZIKI malkia wa pop,  Madonna Louise Ciccon amenunua nyumba ya kifahari kwa pauni milioni 6.8 sawa na zaidi ya sh bilioni 20 za Tanzania, mjini  Lisbon, Ureno ili kukaa na kumsapoti mwanaye aliyemwasili nchini Malawi, James Banda (11)amepata nafasi ya kucheza soka katika kituo cha klabu ya Benfica.

Madonna akiwa na David Banda

David Banda amepata nafasi hiyo baada ya kufanyiwa majaribio na kuonekana kuwa na kipaji, Madonna ambaye amekuwa akifanya shughuli za muziki Marekani kwa kuwa hana matatizo ya fedha ameamua kununua nyumba Ureno ili kuachana na mambo ya kufikia hotelini anapokwenda kumwona mwanaye huyo.
Nyumba aliyonunua ni ya kizamani lakini nzuri, ilijengwa 1865, ina eneo la gereji ambalo gari nne zinaweza kuegesha na sehemu nyingine kwa ajili magari ya wageni kama 20, iko katika eneo la ekari tano, ina vyumba vinne vya kulaa, mabafu saba.
Nyumba hiyo ina ghorofa nne, iko katika eneo la Sintra, umbali wa maili 20 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Ureno, Lisbon, imepakwa rangi ya machungwa.
Nyota huyo kwa sasa yuko nchini humo akiishi hotelini, katika miezi ya karibuni aliweka picha zake kwenye ukurasa wake wa mtandao Instagram  zinazomwonesha akiwa mapumzikoni nchini Ureno.
Madonna akiwa na familia yake yote.

Jarida la nchjini humo, Visao  hizi karibuni liliandika habari, ''Madonna si mtalii, kwa sasa anaishi Lisbon"  na yote hiyo ni kwa ajili ya kipaji cha mpira wa miguu cha mwanaye.
David, ambaye aliasiliwa na Madonna kutoka Malawi mwaka 2006 pamoja na Mercy James amejiunga na kituo cha soka cha Benfica kilichopo katika mji wa Seixal, uliopo nje kidogo ya jiji la Lisbon.
Atabakia katika kituo hadi atapoanza shule katika shule ya Kifaransa mjini Lisbon.
Banda ni mmoja kati ya watoto wanne wa Madonna aliowaasili Malawi  baada ya  Februari mwaka huu kupewa kibali mahakama ya nchini humo cha kuwaasili pacha. Pia ana watoto wawili wa kuwazaa mwenyewe.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...