Skip to main content

Madonna ahamia Ureno kumsapoti mwanaye Mmalawi aliyejiunga na akademi ya Benfica






Picha  iliyopigwa  Aprili 2, 2013 ikimwonesha Madonna (wapili kushoto) akiwa na mwanaye wa kumzaa na aliowaasili (kuanzia kushoto kwenda kulia), David Banda, Lourdes, Mercy James na Rocco  walipokuwa katika Shuke ya Msingi Mkoko iliyojengwa kwa kutumia mfuko wake na kushirikiana na taasisi ya ya Marekani BuildOn, katika Mkoa wa Kasungu, nchini Malawi. Mahakama ya Malawi Februari 7, 2017 ilitoa kibali kwa Madonna kuwaasili watoto wawili pacha wasichana, na kufanya idadi ya watoto aliowaasili kutoka nchini humo kuwa wanne.( PICHA NA AFP)


LISBON, Ureno
NYOTA wa muziki wa pop Madonna  amehamia katika mji wa Lisbon, Ureno ili kuungana na mwanaye aliyemuasili kutoka nchini Malawi, David Banda ajiunge na shule ya mpira wa miguu (academy) ya timu ya Benfica, taarifa zimesema.
“Madonna si mtalii tena, kwa sasa anaishi  mjini Lisbon,” Jarida la kila wiki la Visao limesema, na kuweka
David Banda alivyo sasapicha nyingi za nyota huyo mwenye umri wa miaka 59 ilizozichukua kwenye akaunti yake ya Instagram wakati alipokuwa akitembelea Ureno katika miezi kadhaa iliopita.

David Banda  ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 11 amekubaliwa na timu ya Benfica kuendeleza kipaji chake kwenye shule yao ya soka iliyopo katibu na mji wa Lisbon.
Madonna amekuwa akiishi hotelini, lakini ameshanunua nyumba katika kijiji cha Sintra, kilichopo kiasi cha km 30  kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Ureno.
Nyumba hiyo iliyojengwa karne ya 19 awali ilikuwa ikiizwa kwa dola milioni 9 ( zaidi ya sh. bilioni 20) na inaweza kuchukua miezi sita kukarabatiwa, kwa mujibu wa Visao.
Banda  aliyeasiliwa na Madonna nchini Malawi 2006, amekwua akifanya mzoezi kwenye kituo cha Benfica kilichopo nje kidogo ya  jiji la Lisbon katika eneo la Seixal, limeripoti gazeti la  Correio da Manha .
Klabu huyo imekubali kumchukua mtoto huyo baada ya kumfanyia majaribio na kuridhika na kiwango chake, atabakia kwenye kituo hivho hadi atapoanza shule katika  shule ya sekondari ya kifaransa iliyopo Lisbon, limesema gazeti la Correio da Manha, ikikariri habari hiyo kutoka katika chanzo kilichopo Benfica.
Banda ni mmoja kati ya watoto wa nne walioasiliwa na  Madonna  kutoka nchini Malawi baada ya kuwaasili wasichana pacha Februari mwaka huu. Pia ana watoto wawili wa kuwazaa mwenyewe.
Madonna si nyota wa kwanza kuhamia Lisbon, Ureno. Wengine ni nyota wa filamu, John Malkovich, Monica Bellucci na Michael Fassbender .

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...