![]() |
| Ludovic Charles (kushoto) akimkabidhi mpira Amissi Tambwe kutokana baada ya kufunga mabao manne katika ushindi wa 6-1 dhidi ya Kiluvya United kwenye mechi ya Azam Sports Federation Cup mwaka juzi. |
Ludovic atasaidiana na Ferdinand Chacha (Mwanza) Abdallah Mkomwa (Pwani) na msimamizi atakuwa Josephat Bulali.
Timu hizo zitaingia kwenye mchezo huo zikiwa na ari kutoka na kushinda michezo yao ya mwanzo, Azam iliishinda Ndanda bao 1-0 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara huku Simba ikiichabanga Ruvu Shooting mabao 7-0 kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Viingilio vya mchezo huo ni Sh. 10,000 kwa eneo la VIP lenye viti 1,000 huku katika mzunguko ni sh 7,000.

Comments
Post a Comment