![]() |
| Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane (kulia) alipomuumiza mlinda mlango wa Man City, Ederson katika mchezo wa Ligi Kuu England Jumamosi ilipita katika Uwanja wa Etihad. Livepool ilifungwa mabao 5-0. |
LONDON, Uingereza
TIMU ya Liverpool imesema itakata rufaa kupinga adhabu ya kufungiwa mechi tatu mshambuliaji wake, Sadio Mane baada ya kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo wa ligi Kuu dhidi ya Manchester City, habari zimesema.
Mane mwenye umri wa miaka 25 alioneshwa kadi nyekundu na refa Jon Moss kwa kunyanyua mguu juu wakati alipokuwa akiwania mpira na mlinda mlango wa City, Ederson katika mchezo ambao Liverpool ilifungwa mabao 5-0 Jumamosi.
Liverpoon inaweza kukata rufaa kuomba adhabu adhabu ya Mane ipunguzwe kwa mechi moja au mbili.
Madai ya kuoneshwa kadi nyekundu kimakosa yanaweza kufanya aondokane katika adhabu, lakini nyota huyo angalau atakosa mechi moja.
Mane aligongana na Ederson dakika ya 37 wakati ambapo Manchester City ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0 .
Mlinda mlango huyo raia wa Brazil kutokana na kugongwa na mguu wa Mane alichanika kwenye shavu na kushonwa, hakuweza kuendelea na mchezo.
awali baada ya mchezo Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alisema haoni kama klabu ingekata rufaa hakuwa na uhakika.
" Ninafikiri kila mmoja anajua kuwa hakumwona mlinda mlango. Hakukuna sekunde ya kumwangalia mlinda mlango. Alikuwa akiufuata mpira haraka iwezekanavyo. Natumaini mlinda mlango hakuumia sana.
"[Sadio] amejisikia vibaya sana. Ameshitushwa na hali ilivyokuwa. Sina uhakika wa uamuzi."

Comments
Post a Comment