![]() |
| Washambuliaji wa Liverpool kuanzia kushoto Roberto Firmino, Phillipe Coutinho na Sadio Mane wakifanya mzoezi kabla ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa leo dhidi ya Sevilla. |
LONDON, Uingereza
KIVUMBI cha Ligi ya Mabingwa kinaendelea leo kwenye viwanja nane tofauti barani Ulaya, huku Liverpool ikikumbuka enzi zake za mafanikio kwa kukutana na Sevilla katika Uwanja wa Anfield, Uingereza.
Liverpool inakutana na Sevilla katika mchezo wa Kundi E, ambayo ilikutana nayo katika fainali ya Ligi ya Europa mwaka jana kula kichapo cha mabao 3-1 ikiwa chini ya Kocha Jurgen Klopp.
Liverpool itaingia katika mchezo huo huku ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa mabao 5-0 katika mchezo wao wa Ligi Kuu England Jumomosi dhidi ya Manchester City, itataka kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele kwenye Kundi E, na kuwafariji mashabiki wake.
Mabingwa hao mara tano wa ligi hiyo, katika mchezo wa leo watamkosa Adam Lallana ambaye ni majeruhi wa nyama za paja na Nathaniel Clyne, lakini inaweza kumtumia, Philippe Coutinho anayeweza kucheza mchezo wake wa kimashindano wa kwanza kwenye timu hiyo msimu huu.
Vikosi ambavyo kocha Klopp anaweza kupanga leo;
Kikosi cha kwanza
Kikosi cha pili
Kocha Klopp anataamua awaanzishe washambuliaji gani kati ya Roberto Firmino, Mohammed Salah, Daniel Sturridge, Sadio Mane, Dominic Solanke, Riyan Kent, Ben Woodburn na Harry Wilson ambao wote wako fiti.
Sevilla haitakuwa na Nolito ambaye ni majeruhi na Johannes Geis naye ameachwa kwenye kikosi cha kocha Eduardo Berizzo.
Hata hivyo timu hiyo itakuwa na Ever Banega na Luis Muriel waliopumzishwa katika mchezo dhidi ya Eibar mwishoni mwa wiki ambao ilitoka suluhu ugenini dhidi ya Huesca.
Mchezo mwingine wa kundi hilo utaikutanisha NK Maribor dhidi ya Spartak Moscow.
Mabingwa watetezi wa mashindano hayo Real Madrid ya Hispania watapambana na Apoel Nicosia ya Cyprus huku
Tottenham Hotspur ya England itaikaribisha Borussia Dortmund ya Ujerumani katika mchezo wa Kundi H.
Ratiba ya mechi nyingine leo zitakazoanza saa 3:45 usiku ni;
Kundi F
Feyenoordvs Manchester City
Shaktar Donetskvs Napoli
Kundi G
FC Porto vs Besiktas
RB Leipzig vs Monaco



Comments
Post a Comment