![]() |
| Philippe Coutinho |
MADRID, Hispania
TIMU ya Liverpool ilitaka dau la pauni milioni 185 (zaidi ya sh. bilioni 536) ilikuwachia kiungo mchezeshaji wao, Philippe Coutinho kuhamia Barcelona katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho, lakini viongozi wa Barcelona wakasema hapana!
Barcelona ilikuwa ikimwinda mchezaji huyo katika kipindi cha uhamisho, iliongeza kasi baada ya timu ya PSG kuvunja mkataba wa Neymar na kumsaini kwa ada ya pauni milioni 200 (zaidi ya sh. bilioni 580).
![]() |
| Mkurugenzi wa Michezo wa Barcelona, Albert Soler |
Coutinho ambaye ni raia wa Brazil hajaichezea Liverpool katika msimu huu na aliomba klabu imruhusu aondoke kujiunga na Barcelona.
Liverpool ilikomaa kwa kuweka msimamo kuwa mchezaji huyo hauzwi.
Barcelona kwa sasa inadai Liverpool ilikuwa tayari kumuuza Philippe Coutinho katika siku ya mwisho ya Uhamisho nchini Hispania.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo
, Mkurugenzi wa Michezo wa Barcelona, Albert Soler alisema Liverpool ilitaka dau la Euro 200 ambazo ni sawa na pauni milioni 185 (zaidi ya sh. bilioni 536) ili mkataba usainiwe.
Soler alisema: 'Jana, baada ya wiki kadhaa za kutoa ofa na kuzungumza, Liverpool ilitaka euro milioni 200. Tulipingana na hilo.'


Comments
Post a Comment