![]() |
| Philippe Coutinho wa Liverpool. |
LONDON, Uingereza
MANCHESTER City na Liverpool zimekodi ndege ili kuwarudisha wachezaji wao waliopo katika timu ya taifa ya Brazil ili kuwatumia katika mechi yao Ligi Kuu England itakayofanyika Jumamosi.
Timu ya Brazil ambayo tayari imefuzu Kombe la Dunia 2018 iko Colombia ambako imecheza na nchi hiyo baada ya Ijumaa kushinda mabao 2-0 dhidi ya Ecuador.
![]() |
| Roberto Firmino wa Liverpool. |
Wachezaji wa City waliopo katika timu hiyo ni Gabriel Jesus,
Ederson na Fernandinho, huku wa Liverpool ni Philippe Coutinho na Roberto Firmino ambao wako kwenye kikosi cha kwanza cha nchi hiyo.
![]() |
| Gabriel Jesus wa Man City |
Klabu hiyo zimefikia makubaliano ya kuunganisha nguvu kukodi ndege ili kuwarejesha wachezaji hao na kuwatumia Jumamosi.
Ndege binafsi imeshakudiwa kuwarejesha wachezaji hao England kutoka Barranquilla, Colombia na kutarajiwa kuwasili kesho asubuhi, kwa mujibu wa MEN.
![]() |
| Willian wa Chelsea |
Chelsea nayo imekubalia kuchengia gharama ili mchezaji wake Willian arejee.
Novemba mwaka jana timu hizo pia zilishirikiina kukodi ndege kuwarejesha wachezaji wao walipokwenda kuitumikia timu yao ya taifa katika mechi za kuwania kufuzu dainali za kombe la Dunia 2018.
Wachezaji hao wa City na Liverpool wote wanatarajwia kucheza katika mchezo wa Jumamosi.




Comments
Post a Comment