LONDON, Uingereza
MLINDA mlango wa Manchester City, Ederson ameonesha kwa mara ya kwanza mishono aliyoshonwa na madaktari baada ya kupata majeraha kwa kugongwa na mguu wa mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane katika mchezo wa Ligi Kuu England ulipigwa Jumamosi kweney Uwanja wa Etihad.
Majeraha hayo yalitokana na shavu lake kukutwa na njumu za winga wa Liverpool, Mane, walipokuwa wakiwania mpira mpira wa juu katika mchezo City ilishinda mabao 5-0.
Mlinda mlango huo mwenye umri wa miaka 24 amesainiwa na City kutoka timu ya Benfica kwa ada ya pauni milioni 35 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 104 katika dirisha la usajili lililopita.
Ederson alishonwa nyuzi nane, awali picha zake zilitoka akiwa amebanwa bandeji katika upande wa shavu lake la kushoto.
Kutokana faulo aliyochezewa dakika ya 37, Mane atafungiwa mechi tatu, lakini timu yake inapanga kukata rufaa kupinga, kwa kuwa tukio hilo ni la bahati mbaya
Kama atafungiwa Mane amabye ni raia wa Senega atakosa mechi za Ligi Kuu
dhidi ya Burnleyna Leicester na mchezo wa Kombe la Ligi.


Comments
Post a Comment