Skip to main content

Kinda Liverpool aongezwa mshahara katika birthday



Ben Woodburn akipongezwa na Kocha Jurgen Klopp kwa kucheza vizuri katika moja ya mechi.

LONDON, Uingereza
TIMU ya Liverpool  imeamua kupandishia msharaha mshambuliaji wake kinda Ben Woodburn  kutoka pauni 40,000 (zaidi ya sh. milioni 117) kwa mwaka hadi 25,000 (zaidi ya sh. milioni 73  kwa wiki kutokana na kufurahishwa na uchezaji wake.
Kupanda kwa mshahara wa Woodburn aliyetokea katika shule ya soka ya timu hiyo wakati akisherehekea miaka 18 ya kuzaliwa kwake, ni jambo la faraja kwa kwake na kuonesha kuaminiwa na kocha Jurgen Klopp.
Wekundu hao wameamua watampa mkataba mpya wa miaka sita mchezaji huyo kinda kwa lengo la kutaka aendelea kuichezea timu hiyo ambaye aliongeza umaarufu wake baada ya kuichezea timu ya taifa ya Wales katika michuano ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018.
Mazungumzo ya kuingia mkataba mpya wa kumfanya kuwa mchezaji kamili wa kulipwa yamefikia hatua nzuri, atakuwa akilipwa pauni 25,000 kwa wiki, atakapotimiza umri wa miaka 18, Oktoba 15 mwaka huu.
Liverpool imekuwa na sera inayotaka wachezaji wanaokuwa na umri wa miaka 17 mshahara wao usizidi pauni 40,000 kwa mwaka ili kuwahamasisha.
Awali Woodburn alisaini mkataba wa miaka mitatu Novemba mwaka jana na kuonesha uwezo mzuri katika mwaka wake wa kwanza.
Kocha Jurgen Klopp amekuwa akimwelezea kama ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ambaye ni hazina kwa baadaye, na uchezaji wake katika timu ya Wales ilipocheza dhidi ya Austria na kufunga  na kisha kutengeneza goli muhimu katika mchezo dhidi ya Moldova, alionesha ubora.
Klopp alionesha kumwamini Woodburn na kumpatia mkataba wake wa kwanza Novemba, huku akisema: “Wow, kinachonifurahisha ni kipaji alichokuwa nacho.''

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...