![]() |
| Lionel Messi katikati akimtoka Ronaldo Kushoto katika moja ya mechi zilizoikutanisha timu za barcelona na Real Madrid. |
LONDON, Uingereza
BONDIA bingwa wa ngumi uzito wa juu duniani, Anthony Joshua amesema kama Cristiano Ronaldo angepanda ulingoni kutwangana na Lionel Messi angemshangilia Ronaldo kwa kuwa yuko vizuri kimwili kutokana na mazoezi.
Ronaldo na Messi ni mahasimu wanaochezea timu hasimu za Rel Madrid na Barcelona na wamekuwa wakishindana na kubadilishana tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka katika miaka tisa iliyopita.
![]() |
| Anthony Joshua |
Nyota wa Barcelona, Messi anaongoza kwa kutwaa tuzo mara tano
huku Ronaldo akitwaa mara nne, Joshua anaamini kama wakipanda ulingoni ni Ronaldo atamtwanga Messi.
Joshua aliiambia YouTube channel COPA90: 'Messi anaweza kukwepa lakini Ronaldo anaonekana kuwa na mapigo kama ya Bruce Lee!
'Unajua ninachomaanisha, unakaa mbali na akinyoosha mkono mmoja unakwisha. Messi kidogo anaonekana kama lilivyo jina lake 'uchafu kitu kilichovunjika,' alisema.
Bingwa huyo wa dunia wa mikanda ya WBA na IBO, pia alisema anafurahishwa na jinsi Ronaldo anavyopenda kazi yake, anavutiwa na historia yake ya kujituma na kujitangaza mwenyewe kwa kazi yake .
'Nimekuwa katika ngumi za kulipwa sasa kwa miaka mitatu, ninafikiri mwanzoni nilikuwa nikijaribu kufanya kila kitu katika ngumi ili kuwa mchezaji wa kulipwa,' Joshua alisema.
'Kumbuka sikuwa nafahamika sana, kwa hiyo nilitakiwa kujitambulisha kwa dunia, kwa hiyo katika miaka mitatu niliweza, kujitangaza na kujitangaza.
'Kwa sasa niko katika daraja ambalo nilikuwa ninataka, sasa ninataka kuweka mtazamo wangu kuwa mpiganaji bora zaidi, nimehamasishwa na Ronaldo,' alisema
Joshua pia amesema kama angeambiwa achague mwanasoka ambaye angependa kupigana naye angemchagua kiungo wa Manchester City, Yaya Toure kwa kuwa ukali wake ni kama dubwi'.
Joshua kwa sasa anajiandaa kutwangana na mpiganaji wa Bulgaria, Kubrat Pulev Oktoba 28 mwaka huu Cardiff katika mbapambano la kuunganiosha mikanda mitatu ya IBF, WBA na IBO.
Ronaldo alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2016 na kuonekana anaweza kutetea taji hilo 2017 baada ya kuisaidia Madrid kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa na La Liga.


Comments
Post a Comment