Skip to main content

Hanover 96 yaongoza Bundesliga

Wachezaji wa Hanover 96 wakishangilia.

BERLIN, Ujerumani
TIMU mpya iliyopanda daraja katika Ligi Kuu ya Ujerumani, Hanover 96 imeongoza Ligi baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Hamburg katika uwanja wa HDI-Arena, Hanover na kuwa juu ya timu za Dortmund na Hoffenheim.

Timu hizo zilikuwa sawa kwa pointi kila moja ikiwa na pointi saba kuelekea wikiendi ambapo Dortmund itacheza na Cologne na Hoffenheim itapambana na Hertha Berlin Jumapili.

Bao la Martin Harnik ndani ya dakika 60 na shuti la karibu la mchezaji aliyetokea benchi Ihlas Bebou katika dakika 81 yalifanya Hanover kupata ushindi wa mabao 2-0 na kuendeleza rekodi yake kwa kutofungwa katika mechi 16 za mashindano yote.

Mabingwa watetezi Bayern Munich wako nafasi ya sita kabla ya mchezo wao dhidi ya Mainz 05 leo.

Ratiba ya mechi za leo na kesho ni kama ifuatavyo;

Jumamosi Septemba 16, 2017
Eintracht Frankfurt v Augsburg Commerzbank-Arena saa 10:30
Stuttgart v Wolfsburg Mercedes-Benz-Arena                       10:30
Werder Bremen v Schalke 04 Weserstadion                       10:30
Bayern Munich v Mainz 05 Allianz-Arena                               10:30
RB Leipzig v Borussia M'gladbach Red Bull Arena                 1:30

Jumapili Septemba 17, 2017
Hoffenheim v Hertha BSC Wirsol Rhein-Neckar-Arena        08:30
Bayer Leverkusen v Freiburg BayArena                                10:30
Borussia Dortmund v Koln Signal-Iduna-Park                         1:00




Msimamo wa Bundesliga 2017/2018

NaTimuPWDLGFGAGDPts
1Hannover 96431051410
2Borussia Dortmund32105057
3Hoffenheim32105237
4RB Leipzig32016336
5Schalke 0432015236
6Bayern München32015326
7Hamburger SV420245-16
8Augsburg31115324
9Borussia M'gladbach31113304
10Hertha BSC31113304
11Eintracht Frankfurt31111104
12Wolfsburg311124-24
13Mainz 0531023303
14Stuttgart310225-33
15Freiburg302114-32
16Werder Bremen301214-31
17Bayer Leverkusen301248-41
18Köln300317-60



Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...