| Nicholas Gyan |
MSHAMBULIAJI mpya wa timu ya Simba, Nicholas Gyan kutoka Ghana amefungua akaunti ya ufungaji mabao katika timu ya Simba kwa kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya timu ya Hardrock ya Pemba, Zanzibar.
Gyan ameichezea Simba mechi yake ya pili ya kirafiki baada ya awali kucheza katika mechi dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda katika Siku ya Simba Agosti 8, mwaka huu na timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Alifunga bao lake dakika pili baada ya kuingia kipindi cha pili kwa kupiga shuti la mbali baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mohamed Ibrahim Mo.
Mabao mengine ya Simba yalifungwa na Mo dakika ya 12, 38, Mwinyi Kazimoto na Said Ndeml.
Mwisho
Comments
Post a Comment