Skip to main content

Dembele nje hadi mwakani Barcelona

Ousmane Dembele 

BARCELONA, Hispania
TIMU ya Barcelona imethibitisha mchezaji wake iliyomsaini kwa ada iliyovunja rekodi ya Dunia,Ousmane Dembele atakaa nje ya uwanja kwa minne kutokana na kuumia goti katika mchezo walioshinda ugenini dhidi ya Getafe.
Dembele mwenye umri wa miaka 20, atasafiri kwenda Finland wiki hii na kufanyiwa upasuaji.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliumia katika mchezo wake wa kwanza katika La Liga katika Uwanja wa Coliseum Alfonso Perez na kulazimika kutoka uwanjani dakika ya 25.
Awali miamba hiyo ya Catalan ilitumaini alikuwa ameumia nyama za paja na angekaa nje  kwa wiki chache, lakini vipimo alivyofanyika Jumapili vimetoa matokeo ambayo hayakutarajiwa, ameonekana kuumia zaidi.
" Vipimo vimethibitisha kwamba mchezaji wa timu ya kwanza Ousmane Dembele alichanika katika mshipa uliopo nyuma ya paja la mguu wa kushoto," Barca imesema taarifa.
"Mchezaji atafanyiwa upasuaji na Dk. Sakari Orava nchini Finland wiki hii. Anatarajiwa kuwa kuwa nje kwa miezi mitatu na nusu na miezi minne."
Baada ya kuondoka kwa Neymar katika timu ya Paris Saint-Germain kwa ada ya pauni milioni 198 zaidi ya bilioni 500, Barca ilitumia sehemu ya fedha hizo kumsaini Dembele kutoka Borussia Dortmund, huku mchezaji huyo wa zamani wa Rennes akimzidi Luis Suarez kuwa mchezaji aliyesainiwa kwa ada kubwa zaidi kwenye klabu.
Barca ililipa euro milioni 105 (sh. bilioni 28) kwa kumsaini Dembele, kulingana na mkataba italazimika kuongeza fedha nyingine na kufikia euro milioni 145 (zaidi ya sh. bilioni 388.5) kulingana na uchezaji wake katika Ligi na mashindano ya Ligi ya Mabingwa
Awali Dembele alichezea mechi ya kwanza Barca, akitokea benchi wiki iliyopita ambapi timu yake ilishinda dhidi ya Espanyol, na kutengeneza bao la tano kwa Luis Suarez.
 Kocha wa Barca, Ernesto Valverde kisha alimwanzisha kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa dhidi ya Juventus katikati ya wiki iliyopita.
Kutokana na kuumia kwake, Dembela atakaa nje ya uwanja hadi mwakani, anatarajiwa kucheza mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya Getafe.
Pia Barca haitakuwa na mchezaji huyo katika mechi zote la Ligi ya Mabingwa hatu ya makundi, na pambano la kwanza la Clasico dhidi ya Real Madrid,Desemba 23, mwaka huu.
Kutokana na kuumia kwa Dembele kutafanya mchezaji mmpya mwingine kwenye timu hiyo
, Gerard Deulofeu kupigania kuingia kwenye timu ya kwanza.
Deulofeu alirejea Barca akitokea Everton kwa ada ya pauni euro milioni 12, lakini baada ya kuwasili kwa Dembele kocha Valverde alikuwa akimtumia pamoja na Lionel Messi na Suarez.
Wachezaji wengine ni wanaocheza nafasi yake ni Paco Alcacer, Denis Suarez  na Arda Turan.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...