![]() |
| Ousmane Dembele |
MADRID, Hispania
KIUNGO mchezeshaji Ousmane Dembele amesema hajuti kuhusu kitendo chake cha kugoma kufanya mazoezi katika timu ya Borussia Dortmund, akisema ilikuwa muhimu kufanya hivyo ili kulazimisha uhamisho kwenda.
Winga huyo wa Kifaransa amehamia Camp Nou kwa ada ya euro milioni105 kwenda Camp Nou, alikosaini mkataba wa miaka mitano, akiwa kama mrithi wa Neymar ambaye amehamia Paris Saint-Germain kwa ada ya pauni milioni 222 ambayo imevunja rekodi ya dunia.
Alipoona kuna kuzungusha katika uhamisho, Dembele aligoma kufanya mazoezi na timu ya Burrusia inayonolewa na Peter Bosz, kitu kilichofanya ashindwa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya Ufaransa.
Hata hivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amesema hajuti na kuongeza kama asingechukua hatua hiyo uhamisho wake usingefanyika.
"Nilikuwa nimetulia," Dembele aliiambia Sport na kuongeza kwa kuwa kuwa alikuwa na mkataba mazungumzo ilikuwa lazima yafanyike kati ya Barca na Borussia.
"Nilijua nilitakiwa kuwa mvumilivu. Niliamua kuacha kufanya mazoezi. Sikutaka kwenda. Niliomba ruhusa nisiende,'' alisema.

Comments
Post a Comment