Skip to main content

Cameroon nje, yaichelewesha Nigeria Kombe la Dunia

Wachezaji wa Cameroon wakishangilia.

YAOUNDE, Cameroon
NIGERIA imekosa kujihakikishia kufuzu fainali za kombe la Dunia 2018 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Cameroon, hata hivyo mabingwa Cameroon wametolewa katika mbio hizo.
Nigeria ilionekana kama ingejihakikishia kukata tiketi ya kucheza mashindano hayo baada ya kupata bao kupitia kwa Moses Simon na kudumu hadi dakika za mwisho liliposawazishwa na Vincent Aboubakar kwa njia ya penalti.
Katika mchezo wa awali  uliopigwa Ijumaa Super Eagles iliifunga Cameroon 'Indomitable Lions' mabao 4-0 mjini Uyo na kupanda juu kwenye msimamo wa Kundi B ambalo linatajwa kama Kundi la kifo.
Kwa matokeo hayo ya sare Nigeria imefikisha pointi 10 , inaizidi Zambia iliyopo katika nafasi ya pili pointi sita , huku Cameroon ikiwa na pointi tatu  Algeria ina pointi moja.

Chipolopolo inaweza kuiongezea presha Super Eagles leo kama ikishinda mchezo wake dhidi ya Algeria, huku timu hizo mbili zitapambana mjini Oyo mwanzoni mwa Oktoba katika mchezo ambao matokeo yake yataamua timu itakayofuzu.

Ratiba ya mechi za leo;


 Septemba 5, 2017

CongovGhanaStade Municipal de Kintele11:30
South AfricavCape VerdeMoses Mabhida Stadium02:00
Cote d'IvoirevGabonStade Bouake02:30
DR CongovTunisiaStade des Martyrs02:30
EgyptvUgandaBorg El Arab Stadium03:00
Burkina FasovSenegalStade du 4-Aout03:00
MalivMoroccoStade 26 Mars04:00
AlgeriavZambiaStade Mustapha Tchaker04:30

Ufuatao ni msimamo wa makundi yote kwa nchi za Afrika zinazowania nafasi za kucheza mashindano hayo;


KUNDI A

NaTimu
PWDLGFGAGDPts
1Tunisia33005149
2DR Congo32017346
3Guinea410347-33
4Libya410338-53

KUNDI B

NaTimu
PWDLGFGAGDPts
1Nigeria4310103710
2Zambia31115414
3Cameroon403137-43
4Algeria301237-41

KUNDI C

NaTimu
PWDLGFGAGDPts
1Ivory Coast32106157
2Morocco31206065
3Gabon302103-32
4Mali301219-81

KUNDI D

NaTimu
PWDLGFGAGDPts
1Burkina Faso31203125
2Senegal31113214
3Africa Kusini31114404
4Cape Verde310225-33

KUNDI E

NaTimuPWDLGFGAGDPts
1Uganda32102027
2Misri32014226
3Ghana302113-22
4Congo301224-21

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...