![]() |
| Benard Paul 'Ben Pol ' |
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol ' maarufu kama kidume ameachia albamu yenye nyimbo 15, iitwayo The Best Ben Pol' itakayoanza kuwa mtaani kesho ikiwa ni siku yake maalum ya kuzaliwa 'birthday'.
Mkali wa R n B anasherehekea siku yake ya kuzaliwa Septemba 8, kesho ameachia albamu hiyo wakati anatimiza miaka nane tangu aanze kujihusisha na muziki wa kizazi kipya nchini.
Akizungumza jana na Jambo Leo, Ben Pol albamu hiyo itajumuisha wimbo wake mpya wa 'Kidume' aliomshirikisha mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Chidinma.
Amesema ameamua kutoa albamu ili kuwa karibu na mashabiki wake ambao bila ya wao asingefika alipo.
Pol alisema albamu hiyo ina nyimbo 15, ikiwa na mchanganyiko wa nyimbo mbalimbali alizofanya kwa kushirikiana na wasanii wenzake wa muziki huo.
Amesema nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ni Kidume, Tatu na Tuliza Boli alizowashirikisha Darasa na Rama Dee.
Miongoni mwa nyimbo nyingine ni Nikikupata, Maneno,Jikubali, Yatakwisha, Sophia, Moyo Mashine, Pete na Phone.
"Mimi kama msanii nguli nchini na Afrika Mashariki niliyefanya kazi yangu kwa miaka minane sasa, naona si vibaya kuendeleza muziki wangu kwa kutoa zawadi ya albamu 'Best of Ben Pol' kwa mashabiki wangu, ikiwa na nyimbo 15 nilizoshikirisha wasanii mbalimbali wkiwemo Darasa na Rama Dee” amesema Ben Pol.
Amesema anaamini kila shabiki atapenda kupata albamu yake hiyo ambayo itakuwa katika Septemba ambao ni muhimu sana kwake.

Comments
Post a Comment