MADRID, Hispania
KINYANG'ANYIRO cha Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi kinaanza leo na kesho kwa kuzikutanisha timu 32, leo zikianza 16 katika viwanja nane tofauti. Mechi zote zitaanza saa 3:45 usiku
Leo msisimko mkubwa kwa mashabiki ni mchezo wa Kundi D kati ya Barcelona dhidi ya Juventus kwenye Uwanja wa Nou Camp huku timu za Olympiakos na Sporting Lisbon nazo zikipambana kuwania pointi tatu.
Barcelona inayonolewa na Ernesto Valverde itaikaribisha Juventus huku ikionekana katika miaka ya karibuni zikiwa na upinzani katika msimu huu tayari zilikutana katika mashindano ya kuwania Kombe la Kimataifa, ambapo Barca ilishinda mabao 2-1, yote (kwa Barca) yalifungwa na Neymar.
2015 timu hizo zilikutana katika fainali ya mashindano hayo Barca kutwaa ubingwa, lakini Juve ililipa kisasi walipokutana katika robo fainali msimu uliopita kwa kupata ushindi wa mabao 3-0 kwa ujumla na kutinga nusu na fainali.
Barca imempoteza Neymar aliyehamia PSG ya Ufaransa lakini itakuwa na Ousmane Dembele iliyomsaini kama mbadala wake kutoka Borrusia Dortmund ya Ujerumani, ambaye ameonesha uwezo mkubwa katika ligi.
Valverde ambaye timu yake imeshinda mechi zake zote tatu katika La Liga na kuongoza kwa pointi tisa, leo atamkosa Arda Turan ambaye ni majeruhi, anaweza kuwa na kiungo Ivan Rakitic, anajivunia safu yake ya ushambuliaji yenye wachezaji kama Lionel Messi, Luis Suarez, Dembele na Deulofeu.
Kwa upande wa Juve itakayoongozwa na mlinda mlango mkongwe Gianluigi , safu yake ya ushambuliaji inatarajiwa kuwa na Higuain, Dybala na Mandzukic ambao wameisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Italia, Serie A ikishinda mechi tatu za mwanzo na kuongoza kwa kuwa na pointi tisa sawa na timu za, SSC Napoli, na
na Inter Milan.
Mchezo mwingine utakaovuta hisia ni kati ya Manchester United dhidi ya FC Basel wa Kundi A kwenye Uwanja wa Old Trafford, Uingereza.
Mashabiki watataka kuona kama United inayonolewa na Kocha Jose Mourinho itaonesha makali yake kama katika Ligi Kuu England, ilipofunga mabao nane katika mechi mbili za mwanzo kabla ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Stoke mwishoni mwa wiki.
Mchezo mwingine wa kundi hilo utazikutanisha timu za Benfica dhidi ya CSKA Moscow.
Katika Kundi B, Celtic inayonolewa na Brendan Rodger itapambana na Paris Saint Germain itakayokuwa na washambuliaji wake wapya, Neymar na Kylian Mbappe iliowasaini katika majira haya ya joto kwenye uwanja wa
Parkhead .
Je, Celtic inaweza kuisimamisha PSG nyumbani kama ilivyowahi kuifanyia Manchester City msimu uliopita kwa kutoka nayo sare ya mabao 3-3 ? Hilo ni swali ambalo jibu lake litapatikana baada ya dakika 90.
Mchezo mwingine wa kundi hilo utaikutanisha
Bayern Munich dhidi ya RSC Anderlecht.
Katika Kundi C, Chelsea itakuwa mwenyeji wa FK Qarabag na Roma itaikaribisha Atlético Madrid.

Comments
Post a Comment