Skip to main content

Bao la kideo la Ajibu laizamisha Njombe Mji

Ibrahim Ajibu katikati,

BAO pekee zuri lililofungwa Ibrahim Ajibu dakika ya 16 limeamua matokeo kati ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya wenyeji wa Njombe Mji kwenye Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe.
Kwa ushindi huo, Yanga imefikisha pointi nne sawa na timu za Simba na  Azam FC baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Lipuli ya Iringa kwenye mchezo wa kwanza nyumbani, Dar es Salaam. 
Hata hivyo Mtibwa Sugar ndiyo kinara wa Ligi hiyo baada ya kuifunga Mwadui bao 1-0 hivyo kufikisha pointi sita baada ya kushinda mchezo wao wa kwanza dhidi ya Stand United.
Ajib alifunga bao hilo dakika ya 16 mpira wa adhabu akipiga shuti la umbali wa meta 30, baada ya kuangushwa kwake.
Yanga, walitawala vizuri mchezo kipindi chote cha kwanza na wapinzani wao kucheza vizuri kipindi cha pili lakini mlinda mlango wa Yanga, Youthe Rostand alikuwa shujaa kwa kuokoa michomo mingi.
Matokeo ya mechi nyingine jana, Singida United ilishinda mabao 2-1 Mbao FC, Kagera iligawana pointi na Ruvu Shooting kwa kufungana bao 1-1, Ndanda iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City na Lipuli iliifunga Stand United bao 1-0.
    
 Njombe Mji; David Kisu, Agaton Mapunda, Remmy Mbuligwe, Laban Kamboole, Peter Mwangosi, Joshua John, Awadh Salum, Hassan Kapalata/Behewa Sembwana, Notikeli Masasi, Ditrim Nchimbi na David Nakpa/Raphael Siame.

Yanga SC; Youthe Rostand, Juma Abdul, Gardiel Michael, Andrew Vincent, Kevin Yondan, Papy Kabamba Tshishimbi, Juma Mahadhi, Thabani Kamusoko/Raphael Daudi, Donald Ngoma/Obrey Chirwa , Ibrahim Hajib na Emmanuel Martin/Yussuf Mhilu. 

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...