![]() |
| Kikosi cha timu ya Azam FC. |
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeanza utaratibu wa kutoa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, mashabiki watahusika katika kuchagua.
Kwa mujibu wa habari zilizotolewa kwenye mtandao wa klabu hiyo, tuzo hiyo itadhaminiwa na Benki ya NMB ambao ni wadhamini wa timu hiyo, itatolewa kila mwezi kwa mchezaji bora aliyefanya vizuri lengo likiwa ni kuhamasisha wachezaji.
Awali ni wadhamini wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) pamoja na klabu ya Simba ndiyo walikuwa wakitoa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ambapo hupatiwa fedha sh. 500,000.
Azam FC imewataka mashabiki kuchagua mchezaji wa mwezi Agosti ambapo azam ilicheza mechi moja na kushinda bao 1-0 dhidi ya Ndanda kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Tuzo hiyo ya kwanza itatolewa Septemba 23 mwaka huu, kabla ya kuanza wa ligi dhidi ya Lipuli utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, kuanzia saa 1.00 usiku.
Pia tuzo hiyo itatolewa kwa timu ya vijana ya Azam FC (Azam FC U-20) kila mwezi kama ilivyo kwa timu kubwa.
Tuzo za Azam B zinadhaminiwa na wadhamini wengine maji safi ya Uhai Drinking Water kutoka Bakhresa Food Products, tuzo hiyo itaitwa ‘Uhai Player of the Month.

Comments
Post a Comment