![]() |
| Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi (kulia) akisikitika baada ya Venezuaele kupata bao. |
BUENOS AIRES, Argentina
MBIO za Argentina kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi zimeendelea kusuasua baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu kibonde kwenye kundi lake Venezuela ambayo nji ya mwisho.
Venezuela wakicheza ugenini walipata bao la kuongoza kupitia kwa Jhon Murillo lakini bao la kujifunga la kipindi cha pili liliipatia pointi moja Argentina.
Kwa matokeo hayo Argentina imeendelea kubaki katika nafasi ya tano kati ya sita huku zikiwa zimesalia mechi mbili, timu nne ndizo zitafuzu moja kwa moja huku ya tano italazimika kucheza mechi ya mchujo dhidi ya New Zealand na itakayoshinda itafuzo fainali hizo.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo la nchi za Marekani ya Kusini, Brazil ambayo imeshafuzu fainali hizo ilitoka sare ya bao 1-1dhidi ya Colombia.
Mshambuliaji wa Chelsea, Willian aliifungia bao la kwanza Brazil kabla ya mshambuliaji wa Monaco, Radamel Falcao kufunga la kusawazisha.
Ushindi wa wa Uruguay wa mabao 2-1 dhidi ya Paraguay umeifanya timu hiyo kushika nafasi ya pili, huku Peru ikiichapa Ecuado na kutinga nafasi ya nne. Timu ya sita kwenye msimamo Chile ilichapwa bao 1-0 dhidi ya Bolivia.
Chile, inazidiwa pointi moja na Argentina, katika mchezo ujao itapambana na Ecuador kabla ya kwenda ugenini kucheza na Brazil katika mchezo wa mwisho.
Argentina iliyo na pointi sawa na Peru, katika mchezo ujao itakwenda kucheza na Ecuador. Mchezo wa mwisho wa Peru utakuwa dhidi ya Colombia.
Katika Kundi la Shirkisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean (CONCACAF) Marekani ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Honduras.
Timu zote mbili zina pointi tisa baada ya kucheza mechi nane huku Marekani ni ya nne na Honduras ya tano. timu tatu za juu zitafuzu moja kwa moja Kombe la Dunia.
Timu ya pili Costa Rica ilishindwa kujihakikishia nafasi Urusi baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mexico ambayo imeshafuzu.
Panama imekuwa ya tatu kwa kuifunga Trinidad na Tobago 3-0.
Hadi sasa nchi ambazo tayari zimefuzu fainali hizo ni Ubelgiji, Brazil, Mexico, Iran, Japan, Jamhuri ya Korea na Saudi Arabia
Msimamo wa Kundi la nchi za CONCACAF
Msimamo wa Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini
| Na | Timu | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
| 1 | Brazil | 16 | 11 | 4 | 1 | 38 | 11 | 27 | 37 |
| 2 | Colombia | 16 | 7 | 5 | 4 | 19 | 16 | 3 | 26 |
| 3 | Uruguay | 15 | 7 | 3 | 5 | 26 | 17 | 9 | 24 |
| 4 | Peru | 16 | 7 | 3 | 6 | 26 | 25 | 1 | 24 |
| 5 | Chile | 16 | 7 | 2 | 7 | 24 | 23 | 1 | 23 |
| 6 | Argentina | 15 | 6 | 5 | 4 | 15 | 14 | 1 | 23 |
| 7 | Paraguay | 15 | 6 | 3 | 6 | 16 | 21 | -5 | 21 |
| 8 | Ecuador | 16 | 6 | 2 | 8 | 24 | 24 | 0 | 20 |
| 9 | Bolivia | 16 | 4 | 1 | 11 | 14 | 34 | -20 | 13 |
| 10 | Venezuela | 15 | 1 | 4 | 10 | 17 | 34 | -17 | 7 |

Comments
Post a Comment