Sergio Aguero akimzunguka mlinda mlango wa Liverpool, Simon Mignolet na kufunga bao la kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu England jana ambao Manchester City ilishinda mabao 5-0 katika Uwanja wa Etihad.
LONDON, Uingereza
BAO alilofunga Sergio Aguero dhidi ya Liverpool katika ushindi wa mabao 5-0 kwenye mchzo wa Ligi Kuu England limefanya afikishe mabao 124 na kuwa mchezaji asiyekuwa wa Ulaya anayeongoza kwa ufungaji mabao kwa wakati wote katika ligi hiyo.
Mchezaji huyo wa Argentina amekuwa Manchester City kuanzia mwaka 2011 , ni miongoni mwa wafungaji wakali katika Ligi Kuu England.
Aguero amewapiku wachezaji kadhaa maarufu waliozaliwa nje ya bara la Ulaya na kuwa juu yao.
Tano Bora
Mchezaji aliye katika nafasi ya tano kwenye tano bora ni nyota wa Nigeria, Yakubu aliyezichezea timu za Portsmouth, Middlesbrough, Everton na Blackburn Rovers na kufunga mabao 95.
Anayeshika namba nne ni nyota wa Togo, Emmanuel Adebayor aliyezichezea timu za Arsenal, Manchester City, Tottenham, Crystal Palace ana jumla ya mabao 97.
Didier Drogba yuko katika nafasi ya tatu kwenye orodha akifunga mabao 104 katika timu ya Chelsea baada ya kusainiwa kutoka Marseille na kochaJose Mourinho mwaka 2004.
Drogba alitwaa ubingwa wa England mara nne akiwa na Chelsea.
Dwight Yorke ambaye alichezea timu za Aston Villa, Manchester United, Blackburn Rovers, Birmingham City na Sunderland yuko katika nafasi ya pili kwa kufungwa mabao123.
Ni wa kwanza Sergio Aguero akifunga mabao 124 kwa Manchester City, tangu awasili kwenye timu hiyo 2011; alitwaa nayo ubingwa wa England mara mbili katika misimu yake mitatu ya kwanza.

Comments
Post a Comment