NEW YORK, Marekani
ZLATAN Ibrahimovic ameshindwa kudhibiti hisia zake kuhusu anamshabikia nani kati kati ya Conor McGregor na Floyd Mayweather ambao wametwangana alfajiri ya leo mjini Las Vegas nchini Marekani, akimwita mpiganaji wa Ireland“Ibrahmovic wa MMA”.
![]() |
| Zlatan Ibrahimovic |
Ibrahimovic alisema kuwa anaamini McGregor ana uwezo wa kumpiga Mayweather pamoja na kwamba anapigana katika mchezo waliouzoea wa ngumi bila ya mieleka na mateke.
Akizungumza na SPORTbible, Ibrahimovic alisema: “Hapa kuna mtu ambaye amekuwa akicheza mchezo mmoja kwa miaka mingi na huyo ni Mayweather.
“Kisha mna mtu mwingine ambaye amecheza mchezo kwa muda mfupi, lakini amejitengenezea jina kubwa.
“Kila kitu alichosema amefanya, katika kesi hii, kuna mtu wa MMA anakwenda kwenye ngumi.
“Kabla, kulikuwa na mtu wa aliyejaribu kucheza MMA aliondoka mara moja.
“Kama mshabiki mkubwa wa MMA, I ninaona pambano hili, sijui. Linakwenda kwenye njia.
"Kuna baadhi ya watu wanaotabiri kwamba Mayweather atashinda kirahisi, kitu ambacho siamini.
"Ninafikiri ni ngumu kupigana. Conor ana nguvu, anaweza kukuangusha kutoka kila kona.
"Yeye ni Ibrahimovic wa mapigano mchanganyiko na mimi ni McGregor ulimwengu wa Mpira wa miguu,'' alisema na kuongeza kuwa anajiamini ana anaweza kushinda.
”



Comments
Post a Comment