![]() |
| Kelvin Yondani |
KOCHA Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga ametangaza kikosi kipya kitakachocheza na Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) , Kelvin ni mmoja wa wachezaji waliitwa tena kwenye timu hiyo.
Alisema timu hiyo ityajindaa kwa mchezo wa kirafiki uliopo katika kalenda ya Fifa , Jumatatu Agosti 28 hadi Septemba 2, mwaka huu ambako Tanzania imekubaliana kucheza Botswana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Septemba 2, 2017.
Katika kikosi hicho cha wachezaji 21, Kocha Mayanga amemrejesha mlinzi wa Yanga , Kelvin Yondani huku nyota kutoka nje ya mipaka ya Tanzania wakiwa ni saba akiwamo nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Ally Samatta.
Kikosi hicho kinachotarajia kuingia kambini kesho Jumapili kuanzia saa 2.00 usiku ni makipa Aishi Manula (Simba), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Yanga).
Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Yanga), Salim Mbonde (Simba) na Erasto Nyoni (Simba).
Viungo ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba), Said Ndemla (Simba), Saimon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa (CD Tenerif/Hispania) na Orgenes Mollel (FC Famalicao/Ureno).
Washambuliaji ni Raphael Daud (Yanga), Kelvin Sabato (Azam FC), Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji) na Elias Maguli (Dhofar FC/Oman).
Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Richard Yomba (Daktari wa timu), Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).

Comments
Post a Comment