Skip to main content

Yanga yaikomelea mabao Singida Utd



   
Mlinzi wa Yanga Kelvin Yongani (kulia) akijaribu kumtoka mshambuliaji wa Singida United, Simbarashe Nhivi katika mchezo wa kirafiki ulipigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo. Yanga ilishinda mabao 3-2. 

MABINGWA  watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga wameibuka wabebe mbele ya
Singida United  kwa kuifunga mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki.    

Mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam jana, ulihudhuriwa na mashabiki wengi waliotaka kuona vikosi vya timu zote na  kutokuwa na mechi muda mrefu.

 Yanga  ambayo imecheza mchezo huo ikiwa imetoka kwenye kambui yake Morogoro ilianza kupata bao dakika ya  5 ya likifungwa na Thaban Kamusoko.

Singida United ambayo imepanda daraja msimu huu imesawazisha dakika tatu baadaye kupitia kwa  Danny Usengimana, baada ya kupokea pasi kutoka kwa Deus Kaseke ambaye katika msimu iliopita aliichezea timu hiyo ya Jangwani.

Singida United inayonolewa na Kocha wa zamani wa Yanga, Hans Pluijm ilipata bao la pili dakika ya 22 lililofungwa na mshambuliaji wake Simbarashe Nhivi na kuifanya timu yake kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-1.

Mabadiliko  yaliyofanywa na Yanga kipindi cha pili yaliinufaisha timu hiyo, walimtoa Emmanuel Martin, Mahadhi na Maka Edward na kuingia Donald Ngoma, Ibrahim Ajibu na Pius Buswita.

 Yanga inayonolewa na kocha Mzambia George Lwandamina ilipata bao la pili na la kusawazisha kupitia kwa  Amiss Tambwe kwa penalti baada ya Mlinda mlango wa Singida kumchezea vibaya, Aaid Ronaldo.

 Huku mashabiki wakiamini kuwa mchezo  huo ungeisha kwa sare, dakika ya 90, Yanga ilipata bao la tatu kupitia  Emmanuel Martin kwa shuti kali na kuwafanya mashabiki wa timu yake kutoka na kicheko uwanjani.  

Yanga imeutumia mchezo huo kwa maandalizi ya wamchezo wa Ngao ya Jamii  dhidi ya Simba Agosti 23 mwaka huu, pamoja na ligi                                                          


Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...